Tuesday 13 August 2013

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza dau la Sh100 milioni kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa za kundi la uhalifu





Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza dau la Sh100 milioni kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa za kundi la uhalifu linalojihusisha na vitendo vya kuwamwagia maji baadhi ya watu yanayodhaniwa ni tindikali.
kamanda KOVA
Hatua hiyo inatokana na vitendo hivyo kushamiri maeneo mbalimbali nchini.
Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema vitendo hivyo havipaswi kuvumiliwa na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwafichua watu hao.
“Nimeamua kuomba fedha hizi serikalini ili nimpe mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa hizo, hatimaye kukomesha vitendo hivi. Kemikali hii imekuwa na madhara makubwa,” alisema Kova.
Hivi karibuni Mkurungezi wa Maduka ya Home Shopping Center, Mfanyabiashara wa Lebonon na raia wawili wa Uingereza walimwagiwa maji yanayodhaniwa ni tindikali.

No comments:

Post a Comment