Tumezoea
kuwaona sana kwenye mitaa mbalimbali ya miji mikuu ya Tanzania sanasana
Dar es salaam, lakini Dr. Cheni na timu yake wameamua kuja na ubunifu
wa kufanya watu waisubirie sana movie yake mpya kwa kuamua kumshirikisha
mchina ndani yake.Mwigizaji Dr Cheni baada ya kumtambulisha Steven shabiki wa damu wa club ya Yanga kwamba yupo kwenye movie yake mpya ya ‘nimekubali kuolewa’ itayotoka hivi karibuni, sasa hivi Cheni amemtambulisha raia mmoja wa China ambae ameigiza kwenye hii movie.
Sehemu ya maneno anayoyasema Dr. Cheni kwenye scene na huyu mchina ni “Nyinyi mmekuja kuwekeza kwenye nchi yetu mnawekeza hadi kwa wake zetu” nisikumalizie stori, tazama video yenyewe hapa chini….
Unapenda kupata stori motomoto kama hizi kila siku na kwa wakati? jiunge kuwa mwanafamilia wa millardayo.com kupitia instagram.com/millardayo facebook.com/millardayo na twitter.com/millardayo na upate stori zote zikiwemo Breaking news kwa wakati.
No comments:
Post a Comment