Sunday 3 August 2014

TOFAUTI KATI YA MWANAUME SHOGA NA UBONGO WA MWANAUME WA KAWAIDA?

Utafiti uliofanywa  wataalamu wa masuala ya jinsia  umeonyesha kwamba kuna mfanano katika hali ya ubongo hususani katika eneo liitwalo hypothalamus kwa wanaume ambao ni mashoga “gay males” na wanawake, sehemu hizi katika ubongo kwa mashoga na wanawake ni kubwa kuliko kwa wanaume wakawaida “straight males”. Ukubwa wa eneo hili katika ubongo unaaminiwa pia kuchangia katika tofauti za kijinsia, tofauti za uwezo wakiakili na uwezo wa lugha au kuzungumza. Na hii ndiyo inayosababisha watafiti wengi kulinganisha uwezo mkubwa wa kuongea “verbal abilities” walionao wanawake na wanaume mashoga “gay males”. Hata hivyo zipo tafiti zilizoongeza kwamba kuna maeneo mengine pia katika ubongo wa mwanaume wa kawaida na mwanaume shoga yanayotofautiana kabisa kwenye mvuto wa kimapenzi. Tafiti hizi zinaonyesha kwamba eneo linalohusika na mvuto wa kimapenzi katika ubongo wa mwanaume shoga huhemshwa au kustuliwa na harufu ya jasho la mwanaume mwenzake wakati hali hii haipo kwa mwanaume wa kawaida.Tafiti hizi zimehitimisha kwamba asilimia 35 ya sababu za mwanaume kuwa au kutokuwa shoga, na mwanamke kuwa msagaji “lesbian” au kutokuwa msagaji husababishwa zaidi na vinasaba “genes” na hizo asilimia 65 zilizobaki hazijapatiwa uhakika wa kisayansi ingawa mazingira yanatajwa zaidi kuhusika – Chris Mauki.

Chris Mauki pia amewasaidia wengi kupitia ushauri wa kisaikolojia (professional counseling) katika maeneo mbalimbali ya maisha kama vile ndoa, mahusiano, matatizo ya kitabia, uzazi na malezi, matayarisho ya kustaafu, ushauri wa mambo ya kazi, namna za kuishuhulikia misongo ya mawazo, na mengine mengi
wasiliana naye kwa ushauri zaidi

No comments:

Post a Comment