FASHION

 Kupendeza Mwanamke ndo mpango

 Hivi ndivyo wanaume wanavyowaona siku hizi, maana tunalamika sana kuhusu jinsi wanawake wanavyopaka makeups zao. Na hizi colour combo ndio kabisaaa...Maybe huwa mnanafanya makosa bila kujua. Jaribu kuzingatia yafatayo ukiwa unajiandaa na swala zima la kujipamba
                                 
     Kwanza kabisa unatakiwa ujue shape ya sura yako.hii itakusaidia kujua aina gani ya nyusi zinaendana na uso wako.ukiangalia kwenye hii picha utaona shape ya uso, inaendana na nyusi aina fulani. 
 Tazama hii picha itakusaidia kujua aina gani ya sura, na aina gani ya nyusi inazoendana nazo.
  Unapoenda kununua foundation yako, ijaribu sehemu ya chini karibu na kidevu, na si mkononi ili uweze kujua kama inaenda na uso wako au la
Unapopaka wanja kwenye macho, inabidi ujue una aina gani ya jicho. Jinsi unavyopaka wanja, ndivyo utakavyobadilisha muonekano wako.Kama jicho lako ni dogo,inabidi upake wanja ambao utafungua jicho lako na kulifanya lionekane kubwa zaidi. Ukitazama picha itakusaidia kujua wanja upi unasaidia vipi muonekano wa jicho lako.

Ile style ya kupaka wanja mweusi kwenye lips imeshapitwa na wakati. Paka lipstic au lipshine yako vizuri basi, muhimu kuchagua lipstic inayoendana na wewe

No comments:

Post a Comment