Tuesday, 8 October 2013

King Majuto alivyoibeba familia yake

 

Ukiniuliza majina ya wachekeshaji au waigizaji wa Movie za vichekesho kutoka Tanzania ambao nawakumbuka kwa harakaharaka basi ujue jina la Mzee Majuto litakua la kwanza.

Ni mzee mwenye umri wa miaka 65 ambae amekua akiigiza kwa zaidi ya miaka 20 lakini mpaka sasa anashikilia rekodi ya kuwa mwigizaji anaeongoza kwa movie zake kuuzika dukani na watu kuzipenda.

Japo na mimi huwa nanunua movie zake nimekua na utaratibu wa kufatilia kujua zipi zinauzika, hapo ndo huwa nakutana na info kwamba Mzee bado yuko gado.

Kingine ambacho kimenivutia kuhusu huyu Mzee ambae makazi yake ni Tanga, ni kwamba ametoa ajira kwa watoto wake nane wa kuwazaa kati ya tisa kwa hiyo wote  hao wanafanya nae kazi ya kuigiza.

Badala ya kulipa kampuni milioni tatu za kitanzania ili irekodi movie yake moja, mzee amenunua vifaa vyake na kuwapa kazi watoto wake, Hamza ambae ni msomi wa chuo kikuu akiwa na degree aliacha kazi Tigo na sasa ndio meneja wake anasimamia kazi zote kwenye mauzo na vitu vingine.

Mohamed ni mwalimu wa waigizaji, Haruna ni cameraman na ndio anahusika kwenye kila shooting, Athumani ni mwanamuziki ambae anahusika kupiga muziki wa movie, Abuu ni dereva wa crew ya Mzee na ni fundi pia wa magari.

Kwa kumalizia namkariri mzee akisema: "Mwingine mdogo wa kike anasoma KG3 bado ila anaigiza vizuri sana, kengine kale kachanga kadogo lakini nako kataigiza tu hakuna jinsi manake ajira hakuna na mke wangu ndio anatupikia chakula tunapokua kambini kuigiza."

No comments:

Post a Comment