Upinzani
wa wachezaji bora wa kizazi hiki cha soka Cristiano Ronaldo na Lionel
Messi umekuwa ukitawala vypmbo vya habari kila kukicha.
Usiku wa jana kulikuwa na mchezo wa UEFA
Super Cup kati ya mabingwa wa UEFA Europa League – Sevilla dhidi ya
mabingwa wa UEFA Champions League – Real Madrid, mchezo amba ulipigwa
jijini Cardiff, Wales.
Matokeo ya mchezo huo ni ushindi wa 2-0 kwa
Real Madrid, Cristiano Ronaldo akifunga magoli yote mawili na kuandika
rekodi nyingine kwenye soka barani ulaya.
Magoli hayo ya Ronaldo yamemfanya atimize
jumla ya magoli 70 kwenye michuano ya ulaya na hivyo kumpita Messi
ambaye ana jumla ya magoli 68.
Mpaka kufikia April 2012, nahodha wa Ureno
alikuwa nyuma kwa magoli 18 kumfikia Messi, lakini ndani ya misimu
miwili amefanikiwa kumfikia Messi na kumpita akifunga jumla ya mabao 29
ndani ya msimu miwili.
Ronaldo sasa anakuwa amefunga magoli 68
kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya na mawili kwenye Super Cup, jumla 70,
akiwa amemfikia nyota wa zamani Juventus na AC Milan Fillipo Inzaghi.
Gwiji wa soka wa Real Madrid ndio mchezaji anayeongoza kwa magoli mengi barani ulaya akiwa ameziona nyavu mara 76.
No comments:
Post a Comment