Saturday 9 August 2014

Mashambulizi ya rindima huko Iraq Jesshi la Marekani Lahusika

Wizara ya ulinzi nchini Marekani imesema kuwa inaendelea kuwashambulia wanamgambo wa taifa la kiislamu kaskazini mwa Iraq.
Taarifa imesema kuwa wanajeshi wa Marekani walitekeleza mashambulizi mengine mawili ya angani ili kuulinda mji wa Irbil ambapo wafanyikazi wa marekani wanapiga kambi.
Mashambulizi hayo yanashirikisha ndege isiyo na rubani pamoja na jengine lililotekelezwa na ndege nne za kijeshi za Marekani katika msafara wa wanamgambo hao na maeneo yao ya kurusha makombora.
Awali katika shambulizi la kwanza tangu Marekani iondoe vikosi vyake nchini Iraq mnamo mwaka 2011,ndege za kijeshi zilishambulia mizinga inayotumiwa na wanamgambo hao kukabiliana na vikosi vya Kikurdi vinavyolinda mji wa Irbil.
Vikosi vya Kikurdi vinasema kuwa wapiganaji hao kwa sasa wameliteka bwawa kubwa nchini Iraq karibu na mji wa Mosul ambalo wanaweza kulitumia kutekeleza mafuriko katika miji kadhaa mbali na kukata usambazaji wa maji na umeme.

No comments:

Post a Comment