Thursday 14 August 2014

MTEJA APORWA NA JAMBAZ IMILIONI 19 AKIELEKEA BENKI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,Camilius Wambura.
Majambazi  wamempora mteja Sh. milioni 19 wakati akipeleka fedha hizo katika Tawi la Benki ya Ecobank lililoko eneo la Mwenge, jijini Dar es Salaam. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura, alisema tukio hilo lilitokea majira ya 11:15 jioni juzi wakati mfanyakazi wa wakala wa fedha, Sham Msuya, ambaye ni mkazi wa Kijitonyama, akipeleka kiasi hicho fedha katika benki hiyo.
 
Alisema baada ya tukio hilo, polisi walifika eneo hilo na kufanikiwa kuokota maganda mawili ya risasi zilizofyatuliwa na majambazi hao. “Tumepata taarifa ya tukio hilo, mfanyakazi aliyeporwa fedha jina lake tunalihifadhi. 

Hakuna mtu aliyejeruhiwa, aliyeporwa tunamshikilia kwa uchunguzi zaidi,” alisema Kamanda Wambura.
 
Kaimu Meneja Mkuu wa Tawi hilo, Boniface Kisetu, alisema mtu aliyefanya tukio alikuwa mmoja na alitumia usafiri wa pikipiki na bastola kufanikisha uhalifu huo.
 
Shuhuda wa tukio hilo, ambaye ni mlinzi wa Kampuni ya Ultimate Security, Mpanduli Deogratius, alisema alinusurika kifo wakati jambazi hilo lilipofyatua risasi, ambayo alisema iliyomkosa na kugonga nguzo nje ya benki hiyo.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment