MOYO unahifadhi mengi! Msichana wa mjini 
asiyeishiwa matukio Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ amefunguka
 kwamba yupo tayari kuzaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond 
Platnumz’ kwani amepata taarifa kwamba anasaka mtoto lakini wanawake 
anaokuwa nao hawataki kumzalia, Ijumaa Wikienda linakupasha.
BILA KUMUNG’UNYA MANENO
Akizungumza na gazeti hili bora la mastaa Bongo akiwa dukani kwake 
Kinondoni jijini Dar, wikiendi iliyopita, Anti Lulu bila kumung’unya 
maneno, alifunguka kwamba hivi karibuni alifuatwa na ndugu wa karibu wa 
Diamond au Dangote kama anavyopenda kujiita na kumuomba afanye jitihada 
azae naye.
MAKUBWA!
Alidai aliambiwa kuwa kila Diamond akimpa kibendi mwanamke, huwa 
mwanamke huyo anakwenda kukitoa bila hata ridhaa yake (Diamond).
“Ndugu wa Diamond alinifuata hapa dukani kwangu akanitaka nizae na 
Dangote kwani anasaka sana mtoto na kila akimpa mwanamke mimba huwa 
anaichoropoa bila kuafikiana naye.“Sababu kubwa ya wanawake hao kutoa 
mimba ni kutokana na mpenzi wa Diamond ambaye ni Wema (Isaac Sepetu) 
kudaiwa kuloga ili mwanamke yeyote asizae naye na kila akimpa mimba 
mwanamke inatoka au anakwenda kutoa mwenyewe bila sababu yoyote,” 
alisema Anti Lulu.
Msanii wa filamu za Kibongo Lulu Mathias.
Pamoja na tetesi hizo, Anti Lulu alisema haogopi lolote kwani 
amejizatiti ndiyo maana amejitokeza hadharani na kutaka kuzaa na 
Diamond.
IMANI
Anti Lulu alisema kwamba anaamini Diamond atamkubali japokuwa 
hawajawahi kuzungumzia hiyo ishu wakiwa pamoja na kwamba walishakutana 
na kuzungumza mambo mengine.
“Nataka na nimejizatiti vilivyo kwa ajili ya kumzalia Diamond ‘kabebi’ kazuriii…
“Nataka nione hiyo kulogwa inakuwaje hao wanaotoaga mimba zake bila sababu?
“Nataka na nimejizatiti vilivyo kwa ajili ya kumzalia Diamond ‘kabebi’ kazuriii…
“Nataka nione hiyo kulogwa inakuwaje hao wanaotoaga mimba zake bila sababu?
MTOTO MZURI
“Naamini mimi nitamzalia mtoto mzuri kabisa kwani nimejipanga tayari na siogopi kitu chochote.
“Diamond hajawahi kunitongoza ila kuna siku moja tulionana maeneo ya Kinondoni halafu nikaja kuambiwa na mmoja wa marafiki zake kwamba aliponiona siku hiyo alinisifia.
“Naamini mimi nitamzalia mtoto mzuri kabisa kwani nimejipanga tayari na siogopi kitu chochote.
“Diamond hajawahi kunitongoza ila kuna siku moja tulionana maeneo ya Kinondoni halafu nikaja kuambiwa na mmoja wa marafiki zake kwamba aliponiona siku hiyo alinisifia.
“Niliambiwa alisema kwamba mimi ni mwanamke mzuri na umbo langu ni 
zuri hivyo naomba akubali tu nimzalie jamani,” alisema Anti Lulu ambaye 
aliwahi kuwa prizenta wa runinga na mwigizaji wa sinema za Kibongo.
BIFU?
Anti Lulu alidai kwamba japokuwa anaamini kabisa kwamba Wema 
atakasirika, hatajali kama mbwai iwe mbwai na yupo tayari kuanzisha naye
 bifu zito.
Staa Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kwenye pozi lenye utata.
Alisema kila mmoja atakuwa na nafasi yake kwa Diamond na kwamba 
kikubwa anataka kuzaa na Diamond halafu amkabidhi mtoto kila mmoja 
aendelee na maisha yake.
NENO!
“Najua Wema atakuwa na bifu na mimi lakini sijali kwa sababu nimeamua
 na yeye ni mpenzi wa Diamond tu siyo mke wake kwani hawajafunga ndoa.
“Angekuwa ni mkewe ndiyo ningeogopa lakini hivihivi sihofii chochote,” alisema Anti Lulu.
“Angekuwa ni mkewe ndiyo ningeogopa lakini hivihivi sihofii chochote,” alisema Anti Lulu.
DIAMOND, WEMA NA PENNY
Diamond aliwahi kuripotiwa kumpa ujauzito aliyekuwa mpenzi wake, 
Penniel Mungilwa ‘Penny’ lakini baada ya muda mfupi ilidaiwa 
kuchoropoka.Pia aliwahi kudaiwa kumpachika kibendi Wema ambaye naye 
ilidaiwa ilichoropoka.
Kwa upande wake Anti Lulu aliwahi kutoka na wanaume kadhaa wakiwemo Bond Bin Sinan na Amani ambao hakufanikiwa kuwazalia watoto.
No comments:
Post a Comment