Wakati wimbo wa MdogoMdogo ukiwa bado unasumbua kwenye
media, Diamond Platinumz anatarajia kurusha mawe mengine mazito zaidi
kwa ajili ya kuwaburudisha mashabiki wake.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Babu Tale ambaye ni meneja wa Diamond
amesema mkali huyo anatarajia kuachia nyimbo mbili kwa mpigo na kwamba
zote zimetayarishwa nje.
“Tusubirie kidogo, baada ya miezi miwili mitatu tutaongea kwa sababu
kuna kazi zinakuja, Diamond anarelease ngoma mbili mfululizo na zote
zimetoka nje. Lakini hatuwezi kueongea sasa hivi hadi muda ufike.” Babu
Tale ameiambia tovuti ya Times Fm.
Inaonekana Diamond hataki kuacha gap, anakandamizia palepale azidi
kwenda juu na kutwaa tuzo nyingi za kimataifa kama alivyofanya mwaka
huu.
No comments:
Post a Comment