Ministry of Natural Resources and Tourism - Tanzan
TAARIFA KWA UMMA
MAADHIMISHO YA SIKU YA UTALII DUNIANI KITAIFA MKOANI MWANZA TAREHE 23 – 29 SEPTEMBA 2013
Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Uongozi wa Mikoa ya
Kanda ya Ziwa pamoja na wadau wa tasnia ya utalii nchini wanayo furaha
kuwakaribisha wananchi wote na wadau mbalimbali katika maadhimisho ya
Siku ya Utalii Duniani kwa mwaka 2013 ambayo Kitaifa yatafanyika Mkoa wa
Mwanza.
Siku ya Utalii Duniani
huadhimishwa tarehe 27 Septemba ya kila mwaka ambapo kila nchi
mwanachama wa Shirika la Utalii Duniani husheherekea siku hii. Kwa mwaka
huu Kimataifa, maadhimisho haya yatafanyika katika Visiwa vya Maldives.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Utalii na Maji – Kulinda Hatma Yetu
(Tourism and Water – Protecting Our Common Future)”. Kwa kuzingatia
kauli mbiu hii, tunawajulisha wadau wote katika nyanja mbalimbali za
uhifadhi mazingira, matumizi ya teknolojia sanifu, wafanyabiashara wa
tasnia ya utalii na maliasili, wadau wa sekta ya maji, taasisi za elimu,
wanasiasa, viongozi na wataalamu mbalimbali kushiriki katika wiki ya
maadhimisho ya utalii duniani.
Shughuli zitakazofanyika ni
pamoja na tafsiri ya kauli mbiu katika Nyanja mbalimbali kama,
mashindano ya uandishi wa insha mbalimbali kuhusiana na mada, michezo na
burudani mbalimbali, maonesho ya utalii, malikale, misitu na masuala ya
uhifadhi kwa ujumla, teknolojia mbalimbali, pamoja na ziara ya
kutembelea Hifadhi ya Saanane.
Wananchi pamoja na wadau wote mnakaribishwa sana kushiriki katika maadhimisho haya.
“Kumbuka Utalii ni nyenzo ya kuhamasisha uhifadhi kwa uhai na ustawi wa Taifa”
Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Maliasili na Utalii,
S.L.P 9372,
DAR ES SALAAM.
Simu: 255-22-2864230
Barua pepe: ps@mnrt.go.tz
No comments:
Post a Comment