Friday, 6 September 2013

Muziki umesababisha Ndoa ya Linex na Mfinland kufutwa



 Muziki umesababisha Ndoa ya Linex na Mfinland kufutwa

 


Kilichokua kinafata ni ndoa ambayo ilikua imepangwa na wote wawili baada ya Linex kukamilisha hatua muhimu ambayo ni kumvisha pete mchumba wake anaitwa Suvi raia wa Finland mwezi March 2013.

millardayo.com imepata nafasi ya kuzungumza na Linex kwenye exclusive interview ambayo amekiri ni kweli imebidi kila mmoja aendelee na maisha yake na mapenzi yao kuisha kwa sababu kadhaa zilizojitokeza.
Sababu kubwa ni Suvi kutaka Linex ahamie Finland moja kwa moja na kwenda kuanza maisha mengine kwenye hiyo nchi ambayo ndio ingekua mara yake ya kwanza kufika, namkariri Linex akisema ‘kwa nia nzuri kabisa imekua ngumu kwangu kukubali hayo maamuzi, nataka kuendelea kufanya muziki wangu nyumbani’
‘Tayari nimetumia miaka zaidi ya 10 kutengeneza jina langu kwenye muziki hapa Tanzania, bongo mimi naishi vizuri na familia yangu naisaidia… sina tatizo la kuhangaikia maisha kwa kiasi hicho cha kwenda kuanza tena, yani ni sawa na mtu ameshaanza chuo mwaka wa kwanza alafu mtu anataka kukurudisha darasa la kwanza’
Sababu nyingine ni ‘mimi nimekua upande sana wa mama yangu, tayari nimeshanunua kiwanja namjengea mama yangu na biashara pia hivyo siwezi kuacha hii mipango isimame kwa sababu ya mapenzi, siwezi kuondoka kwenye maisha yangu kwenda kwenye maisha mengine sababu ya mapenzi’
Linex na Suvi walikua wamepanga kuoana lakini kwanza ilikua Linex anatakiwa kwenda Finland kutambulishwa manake ndugu wa mke mtarajiwa walikua wanamsikia tu hawajawahi kumuona, kisha angekwenda Finland kufunga ndoa alafu arudi tena Tanzania kufanya sherehe kisha aondoke moja kwa moja kuhamia Finland’
Ndoa ilikua inatakiwa kufungwa kabla ya february 2014 ambapo uhusiano wao umedumu kwa miaka miwili… baada ya kukutana kwa mara ya kwanza kwenye ndege Linex akitokea Nairobi ambapo Suvi  alikua anatokea Finland na kuja Tanzania/Afrika kwa mara ya kwanza, Linex akamfanyia ukarimu ikiwa ni pamoja na kumpeleka mpaka hotelini’
Kwa kuwa Suvi hakuwa na simu kwa wakati huo, Linex alimwachia namba ya simu lakini Suvi alikua kimya kwa kipindi chote cha mwezi mmoja mpaka siku moja Linex alipokutana nae Mlimani City Dar es salaam ndio urafiki ukaanza, Linex akawa anamtembelea hotelini na Suvi akawa anakwenda nyumbani kwa Linex kwa kipindi cha miezi minne ndio wakaingia mapenzini.

No comments:

Post a Comment