Saturday 28 September 2013

MISS TANZANIA AFANYA KWELI HUKO MISS WORLD,SOMA HAPA

Picture
Picha kutoka kwenye video (imepachikwa hapo chini) ambayo imempa ushindi Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred Lyimo katika shindano hilo.
Wakati warembo 131 leo wanawania taji la urembo wa Dunia (Miss World),  Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred Lyimo ameng’ara kwa kushinda nafasi ya tatu katika kipengele cha Urembo wenye malengo maalum (Beauty With Purpose).

Mrembo huyo amewashinda warembo 129 waliwania taji hilo ambalo ni kubwa baada ya lile la Miss World. Kilichompa ushindi mrembo huyo ni mradi wake wa kujenga bweni la watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambao upo Buhangija mkoani Shinyanga umemgharimu mrembo huyo zaidi ya sh milioni 60.

Katika mashindano hayo, mrembo wa Nepal, Ishani Shrestha alishika nafasi ya kwanza na ya pili ilishikwa na mrembo wa 
Australia, Erin Holland.  Warembo wengine waliomaliza katika 10 bora ya mashindano hayo ni  NoĆ©mie Happart (Ubelgiji) aliyeshika nafasi ya nne, Sancler Frantz (Brazil namba 5), Marine Lorphelin (Ufaransa) nafasi sita.

Pia katika oridha hiyo ya washindi wapo warembo wa Ghana, Uingereza, India na Aruba ambao walishika nafasi ya saba, nane, tisa na ya kumi.

Katika kipengele hicho, warembo hao walifanya kazi za jamii ambazo zina mtazamo wa kimaifa ambapo mbali ya kufanya, mrembo husika anatakiwa kutoa maelezo ya mradi huo mbele ya majaji. Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga alisema kuwa matokeo hayo ni faraja kwa mashindano ya Miss Tanzania kwani yameiweka Tanzania katika chati ya hali ya juu Duniani.

Lundenga alisema kuwa Brigitte ambaye pia ni Miss Sinza aliweza pia kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini na sura nzima ya Tanzania katika mashindano hayo makubwa ya urembo duniani.

 “Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kufanya vyema katika mashindano ya dunia  baada ya Nancy Sumari mwaka 2005 alipomaliza katika fainali ya warembo tano bora kati ya warembo 120 duniani. Nancy alishinda taji la mrembo bora wa Afrika, hivyo Brigitte ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri  leo katika fainali mashindano hayo (Miss World) yanayofanyika mjini Bali, Indonesia, naomba tumuombee aibuke kidedea,” alisema Lundenga

No comments:

Post a Comment