Tuesday, 8 October 2013

Kipya kuhusu Rais Kikwete kukutana na viongozi wa upinzani


IkuluUnaambiwa ofisi ya Rais Ikulu imeanza mawasiliano na viongozi wa vyama vya siasa Tanzania ambavyo vina hoja kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba uliopitishwa karibuni na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nia ya kuandaa mkutano kati ya Rais Jakaya Kikwete na viongozi wa vyama hivyo.
Mawasiliano hayo yameanza Jumatatu ya Oktoba 7 2013 kutokana maelekezo ya Rais Kikwete kwenda kwa Ofisi ya Katibu wa Rais.
Kutokana na matukio yaliyotokea bungeni wakati wa kujadiliwa na kupitishwa kwa Muswada huo mwezi uliopita na kauli mbalimbali ambazo zimetolewa na wabunge wa vyama vya upinzani kufuatia kupitishwa kwa muswada huo na Bunge.
President Kikwete kwenye hotuba yake kwa wananchi Oktoba 4 2013 alisema hoja na kauli za wanaopinga Muswada huo zinazungumzika kwa nia njema ya kutafuta mwafaka katika mchakato wa kutafuta Katiba Mpya.
Kupitia kibonde24.com kwenye sentensi nyingine kuhusu maandalizi ya Rais Kikwete kukutana na viongozi hao, Ofisi ya Rais, Ikulu inaangalia uwezekano wa kuitisha mkutano huo Jumapili ya Oktoba 13 au Jumanne ya Oktoba 15 2013.

No comments:

Post a Comment