Tuesday 21 January 2014

Hatimaye Mapenzi Yasababisha Mpenzi wa Prezoo Kuanika Madudu ya Prezooo kwa Diamond Platnum


starlisha Mpenzi wa Prezzo Stalisha Tillya a.k.a Chagga Barbie

Wakati mapenzi yanaanza kuchanua kati ya Rapcellency Prezzo na mrembo wa kichaga kutoka Tanzania Starlisha Tillya a.k.a Chagga Barbie mwaka jana, wengi tulidhani huenda zile drama zilizojitokeza kwa wapenzi wa rapper huyo waliopita zingepungua au kuisha kabisa, lakini tayari kuna bomu limeshalipuka.Huwa wanasema penzi ni kikohozi sababu kulificha huwezi ndio maana tulishuhudia jinsi mapenzi yalivyokuwa moto moto, na kama ni hivyo pia penzi ni kama chafya yakiharibika si rahisi kuficha cheche za kutoka ndani.

Prezzo na Starlisha
Kupitia Instagram mpenzi wa Prezzo Chagga Barbie leo amevujisha moshi unaofuka ndani ya uhusiano wa wawili hao, kwa kupost ‘private message’ walizokuwa wakichat kabla ya mambo kuharibika.
pz
Alipost picha hii na kuandika, ‘Y nime post baadhi ya chat ni kwasababu umeanza kwa kushare kwa dada zako sasa ntarusha voice note watu wakusikie live ulivyokuwa stupid mwanaume tumamu ha act Kama K*ma kaa wewe, eti hapa ulikuwaukijibabishaaaaa lol unajua hapa nilipokuangalia ndipo nilianza kustuka nikasema huyu babu mwenye rangi za blonde kaa mie nafanya nae nini?’ Ameandika Chagga Barbie muda mfupi uliopita.

Moja ya message hizo inaonesha kuwa Prezzo na mpenzi wake walikuwa wakimjadili Diamond Platnumz ambaye mwaka jana waliwahi kuwa na beef ambayo baadaye iliyeyuka

No comments:

Post a Comment