Tuesday 21 January 2014

MWANAJESHI FEKI ATIWA MBARONI TANGA AKITAKA KUMTAPELI MKUU WA WILAYA...!!


'Koplo feki' akihojiwa wa Luteni Yahya Wangwe na Mteule daraja la pili Albano Semfuko.

VIKOSI vya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa, vinamshikilia Edwin John Mponji (31) kufuatia kwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga na kujitambulisha kwamba yeye ni Koplo wa Jeshi la Wananchi JWTZ akitaka kijana wake afanyiwe mpango wa kuingizwa Jeshi la Kujenga Taifa.
"Koplo" Mponji alikwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego Januari 16 mwaka huu siku ambayo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa ilikuwa katika zoezi la kuwafanyia usaili vijana wanaotakiwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mponji alijitambulisha kuwa yeye ni Ofisa wa JWTZ ambaye kwa sasa yupo kikosi cha 36 KJ Mkoani Pwani ambapo aliambatana na kijana Emmanuel Joseph akitaka afanyiwe mpango ili apate nafasi.


'Koplo feki' wa JWTZ akiwa ofisini kwa Mkuu wa Wilaya.
'Koplo feki' akijiandaa kupanda kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.
Hata hivyo wakati akitoa maelezo hayo, Mshauri wa Mgambo wa Wilaya ya Tanga, Sir Meja Albano Semfuko alimtilia shaka na kumjulisha Mkuu wa Wilaya ambaye aliamuru ashikiliwe kwa mahojiano zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Tanga alisema baada ya mahojiano ilibainika kuwa Mponji si askari wa JWTZ ndipo akalazimika kupelekwa nyumbani kwake mtaa wa Magomeni jijini hapa alipopekuliwa alikutwa na sare za JWTZ zikiwa na cheo cha koplo...

No comments:

Post a Comment