Tuesday 21 January 2014

NDANI YA MPINGO HOUSE SHANGWE MAPOKEZI YA MHE.LAZARO NYALANDU NA NAIBU WAKE MHE. MAHMOOD MGIMWA

WAZIRI MPYA KATIKA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MHE. LAZARO NYALANDU NA NAIBU WAZIRI MPYA MHE. MAHMOOD MGIMWA WAPOKELEWA KWA SHANGWE MAKAO MAKUU YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII JIJINI DAR ES SALAAM.



MHE. lazaro Nyalanu na mke wake

Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya mapokezi ya Mawaziri wake wapya leo Jumanne 21 Januari 2014, ambapo watumishi waliopo Makao Makuu ya wizara wamepata fursa ya kukutana na kufanya maongezi na mawaziri hao.

Mapokezi hayo yanafuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzanaia Mhe. Jakaya Kikwete siku ya Jumapili tarehe19/ 01/1014.

Naibu Waziri Mhe. Mahmood Mgimwa amewaahidi wafanyakazi wa Maliasili na Utalii kufanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu ili kuweza kuleta maendeleo ambayo wananchi wanayategemea kutoka katika Wizara hii.

Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu amewakikishia wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kufanya kazi kwa ushirikiano na weledi ili kuweza kuifanya Wizara kuongeza pato la Taifa kupitia Utalii.

Aidha, Mhe Nyalandu amewaasa watumishi wote kudumisha amani na upendo katika maeneo yao ya kazi ili kujenga mazingira mazuri ya kazi na kuongeza ufanisi..

No comments:

Post a Comment