Jana Rais Jakaya Mrisho Kikwete alitangaza mabadiliko mbalimbali aliyoyafanya katika Baraza La Mawaziri. Rais alitangaza mabadiliko hayo kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi-Ikulu, Balozi Ombeni Sefue katika mkutano na waandishi wa habari na taarifa iliyosambazwa katika vyombo mbalimbali vya habari.
Mabadiliko hayo ambayo Rais ameyafanya kutokana na madaraka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 55 (4) cha Katiba yametokana kitendo cha kujiuzulu au kuwajibishwa kwa mawaziri wanne kujiuzulu mwezi Desemba kufuatia kashfa ya Opereshi Tokomeza ambapo Kamati ya Bunge iligundua kwamba palikuwepo na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na utekelezaji wa hovyo wa opereshi hiyo iliyokuwa imelenga katika kupambana na wawindaji haramu wa maliasili zikiwemo pembe za ndovu.
Mawaziri waliojiuzulu mwezi Desemba ni Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Shamsi Vuai Nahodha(Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Dk. Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi) na Dk. Mathayo David (Mifugo na Uvuvi). Pia mabadiliko hayo yanatokana na kifo cha aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dr.William Mgimwa aliyefariki mwanzoni mwa mwaka huu. Dr.Mgimwa alifia nchini Afrika Kusini alipokuwa amepelekwa kwa matibabu.
Katika mabadiliko yaliyotangazwa, nafasi iliyoachwa wazi na Marehemu Dr.William Mgimwa inachukuliwa na aliyekuwa Naibu wake, Mh.Saada Mkuya Salum. Mh. Saada anakuwa miongoni mwa manaibu waziri kadhaa waliopandishwa vyeo na kuwa mawaziri kamili.
Baadhi ya sura mpya kama ambavyo zinavyoonekana katika picha iliyopo katika post hiyo hapo chini ni Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi), Juma Nkamia (Kondoa Kusini), Jenister Mhagama (Peramiho), Godfrey Zambi (Mbozi ), Pindi Chana (Viti Maalumu), Kaika Telele (Ngorongoro ) Mahmoud Mgimwa (Mufindi Kaskazini) na Dk. Kebwe Stephen Kebwe (Serengeti).
Walioachwa kwenye baraza ni waliokuwa Naibu Waziri Viwanda na Biashara, Gregory Teu, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Goodluck Ole Medeye. Wengine ni aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Theresia Huvisa, na Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi, Benedict Ole Nangoro (Kiteto).
Pia katika mabadiliko hayo Naibu Mawaziri watatu wamepandishwa vyeo kuwa mawaziri kamili ambao ni Saada Mkula Salum (Fedha), Dk. Seif Rashid (Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii) na Lazaro Nyalandu (Maliasili na Utalii).
Hii hapa ndio picha kamili ya Baraza Lote la Mawaziri wakiwemo Mawaziri na Manaibu Mawaziri.
WAZIRI MKUU: MH. MIZENGO PINDA
OFISI YA RAIS [PRESIDENT’S OFFICE]
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-[Utawala Bora]–Mh.Capt.GEORGE MKUCHIKA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais [Menejimenti ya Utumishi wa Umma] - Mh.Celina Kombani
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais [Mahusiano na Uratibu]-Mh.Stephen Wasira
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais [Waziri Asiye na Wizara Maalum] Prof. Mark Mwandosya
OFISI YA MAKAMU WA RAIS [VICE PRESIDENT’S OFFICE]
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais[ Mazingira]- Dr.Binilith Mahenge
Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais [Mazingira] Ummy Ali Mwalimu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais [Muungano]- Mh. Samia Suluhu
OFISI YA WAZIRI MKUU [PRIME MINISTER’S OFFICE]
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu [Uwekezaji na Uwezeshaji]- Dr.Mary Nagu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu [Sera, Uratibu na Bunge] Mh.William Lukuvi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu [TAMISEMI]- Mh.Hawa Ghasia
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Mh. Aggrey Mwanry
WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA
WAZIRI: Mh.Eng. Christopher Chiza
NAIBU WAZIRI: Mh.Godfrey Weston Zambi
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
WAZIRI: Mh. Sophia Simba
NAIBU WAZIRI: Dr.Pindi Hazara Chana
WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
WAZIRI: Prof.Makame Mbarawa
NAIBU WAZIRI: Mh. January Makamba
WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA
WAZIRI: Dr.Hussein Ali Mwinyi
WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
WAZIRI: Mh.Samuel Sitta
NAIBU WAZIRI: Dr. Abdulla Juma Abdulla
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
WAZIRI: Dr. Shukuru Kawambwa
NAIBU WAZIRI: Mh.Jenista Joakim Mhagama
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
WAZIRI: Mh.Sospeter Muhongo
NAIBU WAZIRI:Mh.Charles Muhangwa Kitwanga
WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI
WAZIRI: Mh Saada Mkuya Salum
NAIBU WAZIRI: Mh.Adam Kighoma Malima
NAIBU WAZIRI [SERA]: Mh.Mwigulu Lameck Nchemba
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
WAZIRI: Mh.Bernard Membe
NAIBU WAZIRI: Mh. Mahadhi J. Maalim
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
WAZIRI: Dr. Seif Seleman Rashidi
NAIBU WAZIRI: Dr. Kebwe Stephen KEBWE
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
WAZIRI: Mh.Mathias M. Chikawe
NAIBU WAZIRI: Mh. Pereira A. Silima
WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO
WAZIRI:Dr. Abdallah O. Kigoda
NAIBU WAZIRI: Mh. Janet Zebedayo Mbene
WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
WAZIRI: Dr. Fenella E. Mukangara
NAIBU WAZIRI: Mh. Juma Selemani Nkamia
WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
WAZIRI: Dr.Asha-Rose Mtengeti Migiro
NAIBU WAZIRI:Angela Jasmine Kairuki
WIZARA YA KAZI NA AJIRA
WAZIRI: Mh.Gaudensia Kabaka
NAIBU WAZIRI: Dr. Makongoro M. Mahanga
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
WAZIRI: Mh.Prof.Anna Tibaijuka
NAIBU WAZIRI: Mh. George Boniface Taguluvala Simbachawene
WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
WAZIRI: Dr. Titus Mlengeya Dismas Kamani
NAIBU WAZIRI: Mh.Kaika Saning’o Telele
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
WAZIRI: Mh.Lazaro Samuel Nyalandu
NAIBU WAZIRI: Mh.Mahmoud Hassan Mgimwa
WIZARA YA UJENZI
WAZIRI: Dr.John Pombe Magufuli
NAIBU WAZIRI: Mh.Gerson Lwenge
WIZARA YA UCHUKUZI
WAZIRI: Dr.Harrison Mwakyembe
NAIBU WAZIRI: Dr.Charles J.Tizeba
WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI
WAZIRI: Dr.Jumanne Maghembe
NAIBU WAZIRI: Mh. Amos Gabriel Makalla
No comments:
Post a Comment