MAMBO HADHARANI: INASEMEKANA HUYU NDIYE MCHUMBA WA JACKLINE WOLPER;SIO SIRI TENA...!!!
'Jacqueline Wolper'
akiwa na mchumba wake wa sasa G. Modo. STAA wa filamu Bongo, Jacqueline
Wolper ameamua kumuweka bayana mchumba wake wa sasa anayejulikana kwa
jina la G. Modo baada ya kukaa kimya muda mrefu tangu alipoachana na
Abdallah Mtoro ‘Dallas’.MAKUBWA HAYA BLOG
Akizungumza
hivi karibuni, Wolper alisema alikuwa kimya kwa muda mrefu kwa ajili
ya kutafakari kwanza maana asingeweza kukurupuka wakati bado
hawajachunguzana tabia vizuri na mpenzi wake huyo. Wolper.
“Kiukweli
nafurahia sana uhusiano wangu wa sasa na siwezi kusema moja kwa moja
kuwa ndiye mume wangu kwa vile najua kila kitu kinaongozwa na Mungu,
ninachokiomba ni ndoto yangu ikamilike tu kwani nahisi niliyempata ni
sahihi kwangu,” alisema Wolper.
Wolper
aliongeza kuwa kama siku Mungu atajalia kwa mpenzi wake huyu
kitakachofuatia ni kwenda moja kwa moja kwa wazazi wa pande zote mbili
ili kupata baraka na ndiyo kitu ambacho anakiomba kila kukicha.
No comments:
Post a Comment