TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Katika Mdahalo ulioandaliwa na Taasisi
ya Mwalimu Nyerere, uliofanyika tarehe04/08/2014 mjini Dar es salaam, aliyekuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko yaKatiba Mzee Joseph Sinde Warioba na baadhi
ya wajumbe wenzake pamoja na mambomengine, walikitupia lawama nyingi Chama Cha
Mapinduzi na Mwenyekiti wake RaisJakaya Kikwete kwa hisia nyepesi, dhaifu na za
kutunga.Mara kadhaa na hata katika mdahalo uliopita, baadhi ya waliokuwa
wajumbe wa Tumeya Warioba wamekuwa wakitumia muda mwingi kujaribu kupotosha
umma nakuwashambulia wote wenye mitazamo tofauti na ya kwao.Inaelekea baadhi ya
wajumbe wa Tume ya Warioba wameufanya mchakato wa Katibakuwa mali yao na kufanya
kila juhudi za kujitengenezea hati miliki ya Katiba.Katika mazungumzo yake Mzee
Warioba na wenzake wamekuwa wakitumia takwimukutetea hoja ya serikali tatu.
Lakini hivi sasa wanahama na kusisitiza kuwa ni busarazao ndizo zilizopelekea
kupendekeza muundo wa serikali tatu. Kimetokea nini?La kusikitisha zaidi ni
kuwa; wamekuwa na msimamo mkali usiokubali kusikiliza nakutoa nafasi
kwa mawazo yoyote yanayotofautiana na ya kwao. Badala yake
wanatumia juhudi kubwa kuwalazimisha Watanzania kukubaliana na maelezo yao
hata kamayanaipeleka nchi pabaya.
No comments:
Post a Comment