Naseeb Abdul ‘Diamond Platinumz’, Nyota wa muziki wa Bongo
fleva,amesema licha ya kutafuta video zenye kiwango, pia dharau
na mapozi ya watayarishaji wengi wa Tanzania yamechangia
kuacha kutengeneza kazi zake nchini.Akizungumza jijini Dar es
Salaam juzi kabla ya kwenda nchini Canada, Diamond alisema mtayarishaji
unalipahela kwanza ndio anakufanyia kazi zako, lakini watayarishaji wa
hapa nchini ukishawalipa, kinachofuata ni usumbufu katika kukamilisha
kazi.
Siwezi kumlipa mtayarishaji milioni 40
alafu aniletee dharau, hajui hiyohela nimeipata vipi. Wengi wao
wamekuwa na dharau kama vile wanafanya
kazi bure, ndiyo maana nimekuwa nikifanya kazi nje ya nchialisema Diamond.
Akifafanua zaidi, alisema unaweza ukamweleza mtayarishaji mfike
studio saa 12 asubuhi, lakini atakuja saa nne.Kwangu
hizo ni dharau, kama unaweza kuachana naye, yaani ukishamlipa hela ndiyo kabisa ni mapozi tu alisisitiza.Diamond, mmoja wa
nyota mahiri wa muziki wa Bongo fleva nchini, kwa sasa anatamba na
ngoma yake ya ‘Mdogomdogo’ aliyoifanyia nchini Afrika Kusini chini ya
mtayarishaji mahiri, Godfather.
No comments:
Post a Comment