Wednesday 13 August 2014

Ufaransa kuwahami wakurdi Iraq.



Rais wa Ufaransa Francois Hollande alipokutana na rais wa Marekani Barrack Obama.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa taifa lake litawahami wapiganaji WaKurdi iliwakabiliane na wapiganaji wa Islamic State kaskazini mwa Iraq.
Kulingana na taarifa katika vyombo vya habari vya Ufaransa ,Rais Hollande amepata ruhusa kutoka kwa mamlaka nchini Iraq kuendelea mbele na mpango huo mahsusi wa kuidhibiti Islamic State.
Wapiganaji wa kikurdi wamekuwa wakipiganaji na wapiganaji wa wanamgambo wa Islamic state ambao wameunda himaya yao kaskazini mwa Iraq pamoja na sehemu za Syria.
Mapigano hayo yamesababisha kutokea kwa maelfu ya wakimbizi katika maeneo hayo Kaskazini mwa Iraq.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa atawahami wakurdi Iraq
Kulingana na vyanzo mbadala tayari Marekani imeanza kutoa msaada wa kijeshi kwa makundi ya Wakurdi wajulikanao kama Peshmerga.
Hatua hiyo ya bwana Hollande inafwatia ombi la wakuu wa jimbo la Kurdistan la kuitisha msaada wa kijeshi.
Mapema leo serikali ya Marekani ilituma washauri 130 wa kijeshi katika jimbo la Kurdistan.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa atawahami wakurdi Iraq
Wanamaji hao makomando wa vikosi maalum wa jeshi la Marekani wanatarajiwa kuwashauri kivita wapiganaji hao wa Peshmerga.
Marekani tayari inaendelea na kampeini ya vita vya hewani dhidi ya IS katika jitihada za kuwazuia wasitawale eneo zima la Kaskazini mwa Iraq.
Kiongozi wa waKurudi Massoud Barzani, ameomba msaada wa kijeshi baada ya Islamic state kutwaa miji kadhaa karibu na jimbo la Kurdistan.

No comments:

Post a Comment