Sunday 24 August 2014

UHAMIAJI: IMEZIFUTA RASIMI NAFASI 228 ZA AJIRA ZILIZOTOLEWA KWA UNDUGU


WIZARA ya mambo ya ndani ya nchi imeamua kuzifuta rasmi nafasi 228 za kazi zilizotolewa na UAMIAJI.
Hililimetokea baada ya kugundulika kuwa waajiriwa wengi waliajiriwa bila usawa na bila vigezo.


WIZARA iliamua kuzifuta nafasi hizi zote 228 kwani baadha ya waombaji walikuwa hawana vigezo wala elimu inayojitosheleza kulingana na nafasi walizoziombea .

Baathi ya waajiriwa ambao wanaonakana kuwa na undugu wa moja kwa moja na waajiri wa UAMIAJI hawakuwa na vigezo kama vile kuwa na umri unazidi miaka 25 ambacho kilikuwa kigezo cha msingi kwa baadhi ya nafasi za kazi kama vile koplo na konstebo.


Pamoja na haya maamuzi ya kuzifutilia mbali ajira hizi WIZARA imeunda tume ya watu watano kufuatilia suala hili kwa kina ndani ya siku 10 kuanzia tarehe 1 mpaka 10 augusti.

No comments:

Post a Comment