Sehemu
ya vifaa vya kubaini hatua za awali za ugonjwa wa Ebola kwa kupima hali
ya joto la mwili kwa wasafiri kutoka nje nchi wanaotumia viwanja vya
ndege vilivyokuwa vimeagizwa na Serikali vimewasili jijini Dar es
salaam.
Vifaa hivyo vinavyohusisha kamera 4 zenye uwezo wa kubaini joto la
mwili wa msafiri kwa umbali wa mita 100 bila kumgusa muhusika
vimewasili leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere jijini Dar es salaam kutoka nchini Afrika ya Kusini
vilikonunuliwa.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa wataalam wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Steven Kebwe
amesema kuwa kuwasili kwa vifaa hivyo ni moja ya juhudi za Serikali za
kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama kwa kuuzuia ugonjwa huo
kuingia nchini.
Amesema vifaa hivyo vitapelekwa katika maeneo ya viwanja vya ndege
na maeneo yanayotumiwa na raia wa kigeni kuingia nchini vikiwemo vya Dar es salaam, Zanzibar, Kilimanjaro,Mbeya na Mwanza.
na maeneo yanayotumiwa na raia wa kigeni kuingia nchini vikiwemo vya Dar es salaam, Zanzibar, Kilimanjaro,Mbeya na Mwanza.
Ameongeza kuwa Serikali inaendelea na mpango wa kuagiza vifaa zaidi
vya kuwezesha shughuli ya upimaji wa afya kwa wasafiri wanaotembea
(scanners) zitakazowezesha kubaini afya za wasafiri wengi zaidi kwa
wakati mmoja bila kulazimu kuwasimamisha.
Aidha, amewataka wataalam hao wa afya kufanya kazi zao kwa weledi
mkubwa kwa kuhakikisha wanawapima abiria wote wanaotoka nje ya nchi bila
kujali hadhi walizonazo ili kuweza kubaini kama wana maabukizi au
dalili za ugonjwa wa Ebola.
“Nataka mfanye kazi yenu kwa kuzingatia weledi wa taaluma yenu na kwa
kuzingatia yale mliyojifunza,mvitumie vifaa hivyo kupima kila abiria
ili kubaini joto lake bila kujali cheo wala hadhi yake maana janga hili
ni kubwa,” amesema Dkt. Kebwe.
No comments:
Post a Comment