Wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha North Carolina nchini Marekani, wanatengeza rangi mpya ya kucha ambayo inaweza
hubadili rangi katika sehemu yoyote iliyo na madawa ya kulevya
yanayotumiwa na wanaume kama mtego kwa wasichana na wanawake kwa ujumla.
Vijana hao wanasema kuwa wanawake hujipata hatarini wanapopelekwa nje au kwenye 'Date' na wanaume wenye nia mbaya nao.
Wanasema rangi hii mpya ya kucha itaweza kuonyesha ikiwa kinywaji kimewekwa dawa za kulewesha kama vile GHB na Rohypnol.
Lengo la kampuni hio inayomilikiwa na wanafunzi
hao ni kubuni teknolojia ambazo zinawapa wanawake uwezo wa kujikinga
dhidi ya ubakaji au dhuluma za kingono.
Ukarasa wao wa Facebook
unasema rangi hio ya makucha inaweza kumlinda msichana au mwanamke
yeyote kwani anaweza kuingiza kidole chake katika kinywaji
alichonunuliwa na mwanamume na kuona ikiwa amewekewa chochote humo kwani
rangi hiyo ya kucha inabadili rangi ikiwa kinywaji kile kina dawa za
kulevya.
Rangi hiyo inatengezwa na kampuni ya wanafunzi
hao inayoitwa....'Undercover Colours' na tayari imependwa sana na maelfu
ya watu ishara ikiwa ukurasa wa Facebook na Twitter wa vijana hao. Lakini hisia mchanganyiko ndizo zimeshuhudiwa zaidi.
Mmoja wa wasichana walioonekana kufurahishwa na ugunduzi huo Adam Clark
Estes anayeandikia Gizmodo, alisema kwenye ukurasa wa Facebook wa
Undercover colours kwamba, ''kuna vitu vingi vya kuchunguza ikiwa
kinywaji cha mtu kimewekwa dawa yoyote ya kulewesha. ''Ila ni vigumu
kubeba vifaa hivyo hasa nyakati za usiku unapokuwa umetoka nje ya
mwanamume.
Jessica Valenti
anayeandikia jarida la Guardian, alisema ''Nafurahi kuwa vijana hawa
wanataka kuzuia ubakaji, lakini kwa kuwa ujumbe huu unaelekezwa kwa
wanawake kuwa wajizuie na ubakaji, sio sawa.''
Jesica anasema kusisitiza kuwa waathiriwa wa
ubakaji ndio wanaopaswa kujikinga kutokana na ubakaji , ni kama
kuwalaumu waathiriwa ambao wengi ni wanawake.
''Tayari wanawake wanafanya kila juhudi kujikinga kutokana na ubakaj,'' asema Tara Culp-Ressler.
Sasa eti kukumbuka kujipaka rangi ya makucha ili
kujizuia na ubakaji kwa kuingiza kidole ndani ya kinywaji, ni jambo
linalopaswa kukemewa.''
Pia la kushangaza ni kundi moja linalopinga
ubakaji kukemea wenye kutengeza rangi hio ya makucha wakihoji je wanaume
watajipaka vipi rangi hiyo, ni vyema kukomesha ubakaji sio tu kuuzuia, bali kuukomesha kabisa.
Kama unavyoona hapa haya ni maoni mseto kuhusu rangi hii ya makucha.
Nini maoni yako? Je unaonaje hali ya mwanamke kuweka vidole kwenye kinywaji chake ili aepuke kubakwa?
No comments:
Post a Comment