Baada ya kurudi kwa kuachia nyimbo mbili mfululizo kwenye Radio, Ali Kiba ameanza kuchukua headlines bongoflevani.
23 August Ali amepiga show yake ya pili toka ukimya wa miaka mitatu ambayo ameipiga Tanga kwenye uwanja wa mpira uliokua umejaa maelfu ya watu kwenye tamasha la Fiesta.
Baada tu ya kuifanya hii show aliposhuka backstage, Ali alisema anashukuru Mungu watu wamempokea vizuri kuanzia show ya kwanza aliyoifanya uwanja wa taifa Dar es Salaam na kwamba video zake mbili zinaweza kutoka mwishoni mwa mwezi huu.
Anasema show yake ya mwisho kuifanya ilikua 2012 ambapo kwenye sentensi nyingine Ali ameahidi huu ni mwendo wa kutopumzika yani, hatopumzika tena kutoa nyimbo hivyo wimbo wake mwingine mpya anaweza kuutoa November mwaka huu.
No comments:
Post a Comment