Akizungumza
leo Jijini Dar es Salaam, Mh. Mkapa amesema tatizo la mgongano wa
kimaslahi miongoni mwa viongozi na watumishi wa umma limekuwa
likijitokeza mara kwa mara hasa kwa wale wenye mamlaka au watoa maamuzi
serikalini wanapokuwa na maslahi katika jambo fulani wanatumia madaraka
waliyonayo kuendeleza maslahi yao binafsi badala ya kutoa kipaombele kwa
maslahi ya umma.
Kutokana na tatizo Mh. Mkapa ameitaka sekretarieti ya maadili ya umma
ya viongozi kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa sheria ya kudhiti
tatizo hilo ambalo amesema kama halitatafutiwa ufumbuzi wananchi
wanyonge wataendelea kukosa haki zao za msingi kutokana na ubinafsi wa
viongozi.
Katika hatua nyingine, Msururu wa michango na gharama zinazotozwa kwa
wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika Manispaa ya Kinondoni
jijini Dar es Salaam, imefanya gharama ya elimu katika shule za umma
katika manispaa hiyo kuwa za juu kuliko hata gharama zinazotozwa na
shule binafsi ambazo elimu ni ya kulipia.
Hayo yamebainishwa leo wakati wa Kikao cha Baraza la Madiwani wa
Manispaa hiyo, ambapo mmoja wa wake ambaye bunge wa Kawe Bi Halima Mdee
ameutaka uongozi wa Manispaa hiyo kufafanua ni vipi inasimamia sera ya
serikali ya elimu bure na kwamba ikibidi itaje kiwango halisi ambacho
wazazi wanapaswa kulipa kwa ajili ya watoto wanaosoma kwenye shule za
umma.
Kwa mujibu wa mbunge Mdee, baadhi ya walimu na kamati za shule
zimekuwa hazitumii ipasavyo michango na gharama hizo, na kwamba katika
nyakati fulani baadhi ya walimu wamekuwa wakitumia fursa hiyo
kujinufaisha wenyewe kupitia msururu wa ada na michango aliyoitaja kuwa
ni mzigo kwa wazazi.
No comments:
Post a Comment