KWA MARA YA KWANZA MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI, ZITTO ZUBERI KABWE AMEIBUKA NA KUZUNGUMZIA UHUSIANO WAKE NA MTANGAZAJI WA CLOUDS FM, LOVENESS MALINZI ‘DIVA’ NA KUFUTA UVUMI MZITO ULIOKUWA UKIZAGAA KUWA WAWILI HAO NI WAPENZI.
Zitto
alifunguka hayo juzi kupitia kipindi cha Mkasi kinachorushwa na
Televesheni ya East Africa ambapo alikanusha kuwa hana uhusiano wowote
wa mapenzi licha ya kudaiwa kutungiwa wimbo na mtangazaji huyo kama
ishara ya penzi lao.“Mh! Kama yeye amenitungia wimbo sijui lakini mimi
sina uhusiano naye wowote wa kimapenzi,” alisema Zitto.
Katika
mahojiano hayo, mheshimiwa huyo alifungukia skendo nyingine
inayomhusisha kutembea na staa wa Bongo Fleva, Mwasiti Almasi na kudai
hakuna ukweli wowote juu ya ishu hiyo.
Alisema
anaumia zaidi kusikia watu wanavyomhusisha kutembea na Mwasiti kupitia
mitandao ya kijamii wakati hakuna ukweli wowote ambapo msanii huyo
wanaheshimiana na kufanya naye kazi kwa karibu ili kumsaidia katika
harakati zake za muziki.
“Naumia
sana kusikia wakinisema na Mwasiti wakati yule ni dada yangu na mbaya
zaidi ni mtu ambaye mara kwa mara nimekuwa nikimsaidia katika shughuli
zake za muziki, hakuna kitu kingine zaidi ya ukaka na udada,” alisema
Zitto.
Aidha,
mheshimiwa huyo mbali na kungumzia mikakati yake ya kisiasa katika
kipindi hicho, aliweka bayana kuwa ni baba wa mtoto mmoja kwa mkewe
aliyemtaja kwa jina moja la Jack, wanamlea mtoto wao vizuri lakini suala
la ndoa bado halijatimia.
No comments:
Post a Comment