Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa na Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dk.
Khamis Kigwangala, akitangaza nia yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania wakati alipokutana na waandishi wa habari ambapo
amesema hajasukumwa na mtu yeyote ila ni yeye mwenyewe ameamua kwa moyo
wake.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa na Mbunge wa Jimbo la
Nzega Dk. Khamis Kigwangala akimtambulisha mke wake Dk. Bayoum Awadh
wakati wa mkutano huo.
Mzee Nasser SAid Mussa baba mzazi wa Dk. Khamis Kigwangallah na mama yake mzazi Mama Bagaile Lumola.
Mzee
Nasser Said Mussa ambaye ni baba mzazi wa Dk. Khamis Kigwangala na mama
yake mzazi Mama Bagaile Lumola na watoto wake Sheila kulia ni Hawa.
Ninaishi nikiamini kuwa hadithi ya maisha yangu ni mfano hai kwa
maisha ya watanzania wengi. Na kwamba, nina deni la kulipa kwa vizazi
vijavyo kwa kuwa mimi ninafaidi matunda ya mti uliopandwa na vizazi
vilivyonitangulia. Naliona jukumu la kuhakikisha vizazi vijavyo
vinafaidi urithi wa Tanzania kuwa ni la kwangu na wenzangu wa kizazi
hiki.
Kazi yangu imenifikisha sehemu nyingi sana za nchi yetu – vijijini na
kwenye majiji, imenikutanisha na watu wa kila aina – matajiri kwa
maskini, wazee kwa vijana – hakuna hata mmoja kati ya watu hawa
anayetegemea Serikali itamtatulia kero zake zote. Wanajua wanapaswa
kufanya kazi kwa bidii ili wasonge mbele – na wana nia ya kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment