Habari
za hivi punde kutoka Mkoani Morogoro zinapasha kuwa basi la Kampuni ya
Airbus lililokuwa likitoka Dar es salaam kwenda Tabora limepata ajali
muda si mrefu eneo la Kiegeya Wilayani Gairo Mkoani Morogoro.
Habari zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi(SACP) Faustine Shilogile amesema ni kweli kuna ajali naye yupo eneo la tukio.
“Ninaomba unitafute baade kidogo kwa taarifa kamili kwa sasa nipo eneo la ajali huku Gairo,” alisema SACP Shilogile.
Tunafuatilia zaidi kuhusiana na tukio hilo ambalo linaelezwa kugharimu uhai wa watu zaidi 10.
No comments:
Post a Comment