SASA ni takribani siku tatu zimepita
tokea mfanyabiasha wa madini ya Tanzanite na mmiliki wa hotel kitali ya S.G
Resort iliyopo jijini Arusha aliyefahamika kwa jina la Erasto Msuya kupigwa
risasi 21 na kumsababishia kifo papo hapo katika eneo la njia panda ya KIA
wakati akitoka Mirerani kuelekea Arusha mjini majira ya mchana.
Mazishi ya kifahari yanaandaliwa na familia ya marehemu
Erasto Msuya ikishirikiana na kamati ya wafanya biashara wa madini ya
Tanzanite, huku ikielezwa kuwa jeneza litakalo tumika kubeba mwili wake
linafunguliwa kwa kutumia “rimoti”
Habari kutoka katika kamati ya mazishi inayoundwa na wafanyabiashara hao wa madini ya Tanzanite, ikiongozwa na kaka mkubwa marehemu Gady Msuya, anasema zaidi ya shilingi milioni mia moja (100,000,000/=) inatarajiwa kutumika kugharamia mazishi ya mfanyabiashara huyo bilionea wa madini yav Tanzanite. Na kaka wa marehemu aliendelea kusema kuwa gari maalumu la kubeba mwili wa marehemu na jeneza vimeagizwa kutoka Nairobi, nchini Kenya kwa gharama ya Shilingi milioni nane (8,000,000/=).
Kiasi hicho cha zaidi ya milioni mia moja kinatarajiwa kuchangwa na wafanyabiashara wenzake wa madini . Pia wanatarajia kulipia magari maalumu yatakayotumika kwenye msafara wa mazishi ya Erasto Msuya yanayotarajiwa kufanyika nyumbani kwake Mirerani, wilayani simanjiro siku ya leo tarehe 13 August 2013.
No comments:
Post a Comment