Mwandishi wa ITV Ufoo Saro amejeruhiwa kwa
risasi baada ya mwanaume mmoja ambaye imeripotiwa kuwa hawakuwa na
maelewano mazuri, katika tukio hilo pia mtu huyo huyo alimpiga risasi
mama yake Ufoo Saro na kufariki.Mwanaume huyo alimpiga Ufoo risasi mbili ambazo zilimjeruhi na kudhani kwamba amemuua na kisha yeye mwenyewe kujipiga risasi na kufariki.
Mambo yote haya yalitokea huko Kimbamba
ambapo taarifa zisiso rasmi zinasema kwamba huyo mwanaume baada ya kuwa
na ugomvi kati yake na Ufoo, alienda kuongea na mama mzazi wa Ufoo.
Baada ya kuona kwamba mama huyo yupo upande wa Ufoo ndiyo akaamua
kutimiza adhma yake hiyo
No comments:
Post a Comment