UTAFITI: HIZI NDIZO FAIDA ZA KUFANYA MAPENZI KIAFYA...!! SOMA HAPA KUZIFAHAMU
Kujamiana (ama tendo la ndoa) ni moja ya mambo muhimu sana katika maisha
ya mwanadamu. Ni ukweli usiofichika kwamba wengi wetu tungependa kuwa
na mwenza ambaye mnaridhishana katika tendo la ndoa. Si hivyo tu, bali
tendo hili huleta maelewano katika uhusiano wowote ule. Lakini, kuna
faida zozote za kiafya za kufanya tendo hili? Ndiyo! Zipo faida kadhaa
zinazotokana na kujamiana. Katika makala hii, nitakueleza faida za
kujamiana kiafya kama ambavyo imewahi kuonekana katika tafiti kadhaa
zilizofanyika sehemu mbalimbali duniani.
1. Hulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo: Wanawake ambao hufika kilele
(orgasm) angalau mara mbili kwa wiki kila wanapojamiana, wana
uwezekano mdogo sana (30% tu) wa kupata maradhi ya moyo tofauti na wale
wasiofikia kilele. Hii ni kwa vile homoni ya endorphin inayotolewa
wakati wa kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na hivyo kumuepusha mtu
na magonjwa wa moyo. Aidha kujamiana angalau mara tatu kwa wiki,
husaidia kupunguza uwezekano wa kupata shambulio la moyo (heart attack)
na kiharusi. Uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo wakati wa kufanya
mapenzi ni mdogo sana, ni asilimia 1 tu ya vifo vyote vinavyotokana na
mshtuko wa moyo ndivyo uhusishwa na kujamiana. Aidha, sababu nyingine
inayoongeza uwezekano wa kupata mshtuko wa moyo ni kuwa na uhusiano nje
ya ndoa ambapo huchangia karibu asilimia 75 ya vifo vinavyotokana na
kujamiana, na karibu asilimia 90 ya vifo hivi hutokea kwa wanaume wazee.
Uwezekano wa kupata shambulio la moyo wakati wa kujamiana huongezeka
ikiwa mtu ana miaka zaidi ya 50, uzito uliopitiliza na matatizo ya afya.
Hii ni sawa na kusema unaanza kufanya mazoezi mazito kwa ghafla wakati
mwili na umri haviruhusu.
2. Huongeza ukakamavu wa mifupa: Wanawake waliokoma kupata hedhi
(menopausal women) ambao pia hujamiana angalau mara mbili kwa wiki wana
kiwango kikubwa cha homoni ya oestrogen mara mbili zaidi ya wale ambao
hawajamiani. Homoni hii husaidia kulinda mifupa na kwa wanawake
waliokoma kupata hedhi wakosapo homoni hii hupata ugonjwa wa mifupa
ujulikanao kama osteoporosis.
3.Hupunguza msongo wa mawazo: Kujamiana hupunguza msongo wa mawazo na
shinikizo la damu na humfanya mtu kupata usingizi mnono. Kufikia kilele
ni sawa na kunywa 2-3mg za dawa ya diazepam (kumbuka diazepam hufanya
mwili kupumzika, muscle relaxant), na hii ndiyo sababu kuu ya kwa nini
watu hupata usingizi mzito baada ya kujamiana. Watu wanaojamiana huweza
kuhimili vizuri msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawafanyi hivyo.
Aidha watu wanaojamiana huwa na kiwango cha kawaida cha shinikizo la
damu kuliko wale wasiojamiana. Pia kuwepo kwa viasili vyaprostaglandins
katika shahawa husaidia kupunguza msongo wa mawazo. Viasili hivi
hunyonywa na sehemu za siri za mwanamke. Shahawa pia zina madini ya
zinc, calcium, potassium, fructose na protini ambavyo vyote ni muhimu
kwa afya njema.
aa-couple-in-bedroom4. Hupunguza maumivu: Kufikia kilele (orgasm) wakati
wa kujamiana ni tiba ya maumivu. Homoni ya Oxytocin inayotolewa kwa
wingi kabla na wakati wa kujamiana pamoja na viasili vya endorphins
hupunguza maumivu ya kichwa, mgongo, kipandauso, baridi yabisi pamoja na
dalili zinazotokea baada ya kukoma hedhi (post menopausal syndrome
symptom).
5. H
upunguza uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume kwa wanaume:
Wanaume walio na umri wa miaka 50 na zaidi na ambao hujamiana mara kwa
mara wana uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume (prostate
cancer) hali inayotokana na kusafisha tezi dume mara kwa mara wakati wa
kujamiana. Aidha kutoa shahawa wakati wa kujamiana mara 21 au zaidi kwa
mwezi kunahusishwa na uwezekano mdogo wa kupata saratani ya tezi dume
kwa wanaume wenye umri mkubwa ikilinganishwa na kutoa shahawa mara 4
mpaka 7 kwa mwezi.
6. H
uongeza uwezo wa kunusa:
Baada ya kujamiana, kiwango cha homoni ya prolactin huongezeka, ambayo
hufanya seli za ubongo (brain stem cells) kutengeneza seli mpya katika
sehemu inayohusika kunusa na kutambua harufu (brain olfactory bulb).
7. H
upunguza uzito na kumfanya mtu kuwa na afya njema:
Kujamiana ni mazoezi mazuri. Wakati wa kujamiana, mapigo ya moyo
huongezeka kutoka wastani 70/dakika mpaka 150/dakika ambayo ni sawa na
mtu anayefanya mazoezi kwa kiwango cha juu. Kujamiana huchoma karibu 200
calories sawa na kukimbia dakika 15 katika mashine ya tredmill.
Mwanamke anayefika kilele huchoma calories 47 zaidi.
8. H
uongeza kinga ya mwili:
Kufanya mapenzi mara moja au mara mbili kwa wiki huongeza kiwango cha
seli za kinga aina ya immunoglobulin A kwa robo tatu, na hivyo kumkinga
mtu dhidi ya mafua na magonjwa mbalimbali.
black-women-beauty-central
9. Kufanya mapenzi huongeza urembo wa mwanamke:
Wanawake wanaojamiana angalau mara nne kwa wiki huonekana kuwa na umri
mdogo ikilinganishwa na umri wao kwa miaka 7 mpaka 12, hii inatokana na
ukweli kuwa kujamiana huongeza homoni ya oestrogen ambayo hufanya nywele
za wanawake kuwa na afya nzuri na ngozi zao kung’aa.
10. Hudhibiti mzunguko wa hedhi kuwa wa kawaida:
Wanawake ambao hujamiana angalau mara moja kwa wiki (isipokuwa siku
ambazo wako kwenye hedhi) huwa na mzunguko wa hedhi wa kawaida
ikilinganishwa na wale ambao hufanya mapenzi kwa nadra au wale ambao
hawafanyi kabisa.
11. Tendo la ndoa huongeza hali ya kujiamini:
Ikiwa litafanyika baina ya wapendao, na tendo lenyewe likawa la furaha
na upendo, kujamiana huongeza kujiamini.
12. Huongeza ukakamavu katika misuli ya nyonga (pelvic floor muscles):
Na hivyo kuzuia mwanamke kupata matatizo ya mkojo au ugonjwa wa kibofu
cha mkojo. Wanawake ambao wamekoma kupata hedhi, kufanya mapenzi mara
kwa mara huondoa tatizo la kusinyaa kwa sehemu za siri za mwanamke
(vagina atrophy) na hivyo kumwepusha na maambukizi katika njia cha
mkojo (Urinary Tract Infection ).
13. Kufanya mapenzi huongeza kasi ya mzunguko wa
damu mwilini:
Unapojamiana na kufikia kilele, mzunguko wa damu huongezeka maradufu,
hivyo kuongeza mzunguko wa hewa aina ya oksijeni kwenda kwenye viungo
muhimu kama moyo, ubongo na figo hivyo kusaidia kuondoa uchafu na sumu
mbalimbali mwilini.
14. H
uongeza hali ya kujithamini au kuthamini mwili wako:
Hakuna kitu kizuri kama mtu kutambua ana maumbile mazuri na ya kuvutia,
haya yote hupatikana wakati mtu yupo uchi wakati wa kujamiana na mwenza
wake kumwambia kwamba ana maumbile mazuri na ya kuvutia, hii huongeza
hali ya kujithamini na kujipenda kwa binadamu yoyote.
15. H
usaidia kuishi kwa muda mrefu:
Kufanya mapenzi angalau mara mbili kwa wiki hurefusha maisha yako. Kila
unapofikia kilele, homoni aina ya DHEA (Dihydroepiandrosterone) hutolewa
kwa wingi kutokana na raha ya tendo na kufikia kilele. DHEA huongeza
kinga ya mwili, hurekebisha tishu zilizoharibika (hutibu vidonda),
huongeza kiwango cha ufanyaji kazi cha ubongo, huiweka ngozi kuwa na
afya bora na hupunguza msongo wa mawazo. Kwa hiyo, kuongeza kufikia
kilele kuna uwezekano wa kurefusha maisha yako.
16. Kujamiana huongeza upendo na msisimko katika mapenzi, kutokana na
kuongezeka kwa homoni ya oxytocin (love hormone), ambayo huleta
mshikamano, uaminifu, na unyenyekevu katika uhusiano au kwenye ndoa.
17. Huongeza uwezo wa kuzaa au kutunga mimba:
Mara nyingi watu huuliza kama urefu wa uume una uhusiano wowote na uwezo
wa kutunga mimba. Jibu zuri ni hapana! Kufanya mapenzi mara kwa mara
huboresha shahawa za mwanamume, huzifanya kuwa katika kiwango kizuri, na
kama unataka kupata mtoto, ni bora kufanya mapenzi mara kwa mara sio
kutumia shahawa zilizokaa kwa muda wa siku nne.
No comments:
Post a Comment