Fernando Torres amemaliza kipindi kigumu kabisa cha miaka mitatu na
nusu kwenye maisha yake ndani ya klabu ya Chelsea baada ya kukubali
kuondoka katika timu hiyo.
Fernando alijiunga na Chelsea mnamo mwaka 2011 January kwa ada ya
uhamisho ambayo ilivunja rekodi ya usajili nchini Uingereza – £50m
akitokea Liverpool – leo hii imethibitishwa rasmi kwamba mchezaji huyo
sasa anajiunga na klabu ya AC Milan ya Italia kwa mkataba wa mkopo wa
miaka miwili.
Torres anajiunga na AC Milan kwenda kurithi nafasi ya Mario Balotelli ambaye amejiunga na Liverpool kwa ada ya uhamisho wa £16m.
Torres ameichezea Chelsea mechi 172 na kufanikiwa kuifungia magoli 45 tangu alipotia mguu Stamford Bridge.
Mchezaji huyo anategemewa kwenda Milan kesho tayari kufanyiwa vipiko vya afya.
No comments:
Post a Comment