Friday, 29 August 2014

KAMPUNI YA MATANGAZO YANAYOTEMBEA (TRIA) YAZINDULIWA RASMI TANZANIA‏


1q
2q
Kampuni ya matangazo kwa kutumia vifaa tembezi yaani matangazo yanayotembea imezinduliwa rasmi jijini Dar esSalaam.
Akiongea na waandishi wa habari pamoja na wageniwengine waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi ulifanyika katika hanga la shirika la ndege la Precision yenye makao makuu yake eneo la uwanja wa ndege jijini Dar esSalaam, mkurugenzi mtendaji na muasisi wa TRIA bw. Trushar Khetia amesema kuwa TRIA ni kampuni ya kimataifa inayojishughulisha na matangazo yawekwayo juu, nje au ndani ya fifaa safirishi kama mabasi ya kusafiria ndani na nje ya miji, ndege na usafiri wa majini maarufu kama boti au meli.
“Tumezoea kuona ama kusikia matangazo malimbali ya kibiashara nay ale ya kijamii yaani matangazo yasiyo ya kibiashara yakifanyika kupitia kwenye TV REDIO magazeti na majarida hapa nchini lakini leo TRIA inawathibishia wafanya biashara wa Tanzania na wengine kuwa matangazo yanaweza kufanyika popote wakati wowote tena kwa gharama ndogo” alisema bwana Trushar na kuongeza kuwa TRIA ina lenga kuwainua watanzania hasa vijana wadogo na kuwafanya watambue fursa zao katika maisha sambamba na kuwaongezea matumaini makubwa wamiliki wa mabasi, ndege, daladala namakapuni ya usafirishaji katika kunufaika kutokana na biashara zao za usafirishaji.
Aidha bwana Trushar amesema kuwa kampuni yake pamoja na kwamba haitegemi kufanya biashara kwa hasara hailengi pia kutengeneza faida tu bali kuleta ufanisi na changamoto endelevu katika sekta ya masoko na matangazo ambapo vijana wadau na wateja wa huduma hiyo wataweza kupiga hatua za kimaendeleo kibiashara sambamba na kuongezeka kwa soko la ajira hususana kwa vijana wa kitanzania “TRIA Tanzania hailengi kutengeneza faida tu bali pia kuleta maendeleo yenye tija kibiashara kwa wale watakaokuwa wateja wetu na wadau kwa ujmla, lakini pia ajira kwa vijana wenye uwezo tofauti tofauti wa kufanya kazi pamoja na wale wenye utaalamu wa kuandaa na kutengeneza matangazo haya” alisema Khetia.
Kwa upande wake mwakili wa Conica katika hafla hiyo Bi Diana Lavender amesema Conoca imekuwa mteja mkubwa wa TRIA nchini Kenya na kwakutambua ubora wa kazi zinafanywa naTRIA Conica imeamua kuunga na TRIA kwakuendelea kufanya matangazo yake hapa chini “tumekuwa wateja wa hii kampuni mda mrefu sasa huko nchini Kenya na kutoka na mafanikio makubwa tumeweza kupata kupitia matangazo yetu yanayofanywa na TRIA tumeonelea kuwa ni vizuri kuja kufanya hayo matangazo hapa Tanzania hasa pale tuliposikia kwamba TRIA inaanzisha tawi hapa nchini” alisema Lavender na kuongeza kuwa kufanya matangazo kupitia mabasi, ndege, daladala, treni, vyombo vya usafiri wa majini ni sehemu ya mapambo ya mji na njia zake kwani matangazo haya hutengenezwa vizuri na kufanya kuvuta macho ya wengi kila ipitapo “ni ma mabasi yetu huko Kenya maarufu kama matatu ukipita ukiona vile inavutia lazima utafurahia na kwamba lazima unaweza kutaka kupanda hiyo basi” aliongeza.
Naye mwakilishi kutoka shirika la ndege la precision hapa nchini ambao ni moja kati ya wadau wa karibu kabisa na TRIA Bi Azda Amani amesema kuwa uwekezaji wa biashara mbalimbali hasa biashara ngeni kama hayo ni sehemu ya kuongeza na kukuza pato la taifa na kupitia kodi kwa kampuni husika lakini pia kwa wamiliki wa mabasi, ndege na vinginevyo pamoja na wale wamiliki wa matangazo yatakawekwa kwenye magari haya watalipia kodi “ni furaha kuona wawekezaji wakubwa na wadogo wakiingia kila siku hapa nchini kuwekeza kibiashara na kwakufanya hivi nchi yetu ina kuwa pia kiuchumi kupitia kodi kutoka kwa watoa huduma na wahudumiwa wa huduma hii muhimu kwa maendeleo ya uchumi na biashara nchini” alisema Amani
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Zulfikar Mohamed kutoka Transpaper ameisifia TRIA kwa hatua iliyofikia na kuwataka watanzania kuiga mfano huo muhimu na kwenda kuwekeza pia katika nchi jirani hata kimataifa “ mimi nipewa fursa ya kuzindua tawi la TRIA hapa Tanzania na kwakweli nimefurahia fursa hii.
Naomba kuwapongeza sana wahusika wote waliokaa na kuona kwamba mimi naweza kuwa mgeni rasmi wa kuzindua mradi huu muhimu lakini pia nawasifia watanzania kwa kuwa waungwana wakubwa sana kuwapokea wawekezaji kutoka pande zote za dunia bila kujali rangi kabila wa udini, kwa hili mko vizuri sana na nawapongeza sana niwaombe tu kwamba igeni huu mfano mzuri na nyinyi mkawekeze biashara zenu katika nchi nyingine kwa manufaa ya watoto wenu na watanzania wote” alisema Mohamed nakuongeza kuwa maendele ya kiuchumi katka taifa lolote huletwa na wenye nchi kupitia biashara yenye tija na inayovuka mipaka na kuleta fedha za kigeni.

No comments:

Post a Comment