Miongoni
mwa vitu ambavyo msanii Jux amekuwa akivikwepa kuzungumzia kila
alipoulizwa ni kuhusu uhusiano wake na Jackie Cliff aliyekamatwa na
madawa ya kulevya mwishoni mwa mwaka jana (2013) nchini China, ambaye
mara nyingi amekuwa akisema ni mshkaji wake tu.
Hivi ndivyo ilivyoandikwa:
MALOVEE!
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, staa wa Bongo Fleva anayetamba na
wimbo wake wa Nitasubiri, Juma Khalid ‘Jux’, kwa mara ya kwanza amevunja
ukimya na kufungukia penzi lake na modo anayedaiwa kufungwa nchini
China kwa msala wa madawa ya kulevya ‘unga’, Jacqueline Fitzpatrick
Cliff ‘Jack Patrick’.
Jux
ambaye anasoma nchini China huku akifanya muziki wa Bongo Fleva,
alifunguka hayo juzikati katika ‘exclusive interview’ aliyoifanya na
mwanahabari wetu alipokuwa mjini Kahama alipokwenda kwenye Serengeti
Fiesta 2014.
Akijibu
swali la mwandishi wetu lililomtaka afungukie penzi lake na Jack ambalo
alikuwa akichengachenga kila alipotakiwa kutoa ufafanuzi na vyombo vya
habari, Jux alianza kwa kukiri kwamba mrembo huyo alikuwa mpenzi wake na
walidumu kwa takriban miezi saba kabla hajakutwa na msala wa madawa ya
kulevya.
Alisema
tangu aanze kuyajua mapenzi, Jack alikuwa ni mwanamke wa pekee kwake
ingawa wakati anapatwa matatizo walikuwa wametibuana kwa kipindi cha
wiki mbili.
“Nilisikitika
sana niliposikia amekamatwa kwa madawa ya kulevya, nilikuwa sijui kama
anafanya hiyo biashara na kinachoniumiza zaidi ni kwamba nilikuwa najua
yupo Bongo na nikajua tutaonana maana mimi nilikuwa Bongo wakati huo,” alisema Jux.
Alipoulizwa kama ana taarifa za Jack kufungwa miaka sita jela kama ilivyoripotiwa wiki iliyopita, Jux alisema hana taarifa hizo.
“Kiukweli sijazipata habari hizo labda nitakapoenda tena China ndiyo nitajua kupitia kwa mwanasheria wake maana kwa sasa hajanipa taarifa na hana namba yangu ya simu ya hapa,” alisema Jux.
“Kiukweli sijazipata habari hizo labda nitakapoenda tena China ndiyo nitajua kupitia kwa mwanasheria wake maana kwa sasa hajanipa taarifa na hana namba yangu ya simu ya hapa,” alisema Jux.
Jack
alikamatwa Desemba 19, mwaka jana akiwa amebeba madawa ya kulevya aina
ya Heroin yenye uzito wa kilo 1.1 katika Uwanja wa Ndege wa Macau
akitokea jijini Bangkok nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa
Jimbo la Guangdong Kusini mwa China.
No comments:
Post a Comment