Sunday 24 August 2014

WAMILIKI DALADALA WASALIMU AMRI KWA UDA

Wamiliki wa mabasi ya daladala wamesalimu amri kwa Kampuni ya Usafiri  (UDA) na kukubali kusaini makubaliano ya kulipwa fidia kwa kutotumia Barabara ya Morogoro, jijini Dar es Salaam.
Barabara hiyo ipo kwenye mradi wa mabasi ya mwendo kasi ulio chini ya kampuni ya (Dart) ambapo mwishoni mwa mwezi huu inatarajia kukabidhiwa.


Makubaliano hayo yalifikiwa jana baada ya pande zote mbili kusaini mkataba kwa masharti makuu mawili ya kulipwa fidia na kuacha magari au kupewa nusu ya fidia ya thamani ya gari na mmiliki kwenda njia nyingine ambayo haijapita maradi huo

No comments:

Post a Comment