Usiku wa Jumamosi Agosti 30, 2014, majira ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa Bongo Flavor, Nasib Abdul maarufu kama Diamond
Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini
Stuttgart, Ujerumani, baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka
kusubiri show.
Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini Stuttgart, Ujerumani. |
Mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi euro
25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini
walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 alfajiri ndipo mwanamuziki
Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anayejiita
Britts Event.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza
kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake,
Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa
katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kuvunja hadi vyombo
vya muziki, ma-Djs walishambuliwa na wapo hospitalini kwa sasa.
Mmoja wa Djs hao alipoteza lap top yake, mwanadada DJ Flor alipatwa
mstuko wa moyo na kukimbizwa hospitali, washabiki hao walimpa kipigo DJ
Drazee naye yupo hoi hospitali. Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio
hili la aibu halijawahi kutokea, kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani
kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa Ujerumani
wanaheshimu sana muda wao.
Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema
wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia
itamfungulia mashataka promota huyo raia wa Nigeria ambaye pia
anachunguzwa kwa kujihusisha na mtandao fulani wa biashara.
No comments:
Post a Comment