KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Paroko Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji Luhanga, Padri Richard D’souza, ameshindwa kufungisha ndoa baada ya bibi harusi kubainika kuwa ni mke wa mtu.
Bibi harusi aliyejulikana kwa jina la Neema Hoza, ambaye alitaka kufunga ndoa na mwanamme mwingine ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, anadaiwa kuwa alishafunga ndoa na Brighton Mhache katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kimara.
Bibi harusi aliyejulikana kwa jina la Neema Hoza, ambaye alitaka kufunga ndoa na mwanamme mwingine ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, anadaiwa kuwa alishafunga ndoa na Brighton Mhache katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Kimara.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki,
kaka wa mume wa Neema, Fadhili Mhache, alisema mdogo wake alikwishafunga
ndoa na Neema, lakini cha kushangaza shemeji yake huyo kutaka kufunga
ndoa tena wakati kikanisa hairuhusiwi.
Mhache,
alisema walifikia hatua hiyo ya kwenda kanisani kusimamisha ndoa hiyo,
kwa sababu Neema alikuwa bado ni mke wa mtu, hivyo hakustahili kuolewa
na mwanamme mwingine na kwamba, aliondoka nyumbani akisema anakwenda
kwa dada yake kupumzika.
“Tunachojua,
aliamua kwenda kwa dada yake baada ya kugombana na mumewe, sababu
ambayo ilimfanya asema anakwenda kwa dada yake kupumzika kwa muda,”
alisema Mhache na kuongeza.
Sisi
tulijua alikwenda kupumzika kwa dada yake, hatukujua kama ana mpango
wa kufunga ndoa, ila tulipata taarifa leo asubuhi kwa majirani zake
kuwa anafunga ndoa na mwanamme mwingine tukaamua kwenda polisi
kuwafahamisha na kisha tukaja huku, ila hawa wawili waliyotaka kufunga
ndoa wote wanaishi Kimara, iweje waje kufungia huku, hapa kuna tatizo
tena kubwa.
Kwa upande wake, Brighton alisema jambo hilo la mke wake kufunga ndoa tena katika kanisa jingine, linamuumiza sana na kumsikitisha.
“Naumia
sana jamani… hata kama tuligombana lakini haukuwa ugomvi ambao
ungemfanya hadi afikie hatua ya kufunga ndoa nyingine kwa mujibu wa
sheria za dini yetu, mimi bado namtambua kama mke wangu halali
niliyefunga naye ndoa katika kanisa la KKKT Kimara,” alisema.
Kwa upande wake, dada wa bibi harusi, Rebeca Hoza, alisema ni kweli mdogo wake alikwishafunga ndoa na Brighton,
hata hivyo tangu wafunge ndoa hiyo, walikuwa hawana maelewano mazuri
ndani ya nyumba.
Alisema
mdogo wake alipata manyanyaso katika ndoa hiyo hadi wakaamua
kupelekana mahakamani ili kuivunja ndoa hiyo, lakini cha kushangaza
tarehe iliyopangwa Brighton kwenda kuandika talaka kwa mkewe, hakufika
mahakamani hapo.
“Mara
nyingi mdogo wangu alikuwa akigombana na mume wake, walikuwa
wanapigana hadi kuvunjana mikono, wakati mwingine alikuwa anamshikia
kisu na kumwambia kuwa atamuua.
“Tumeenda
mahakamani lakini alishindwa kuja kuandika talaka na ni miaka mitatu
sasa, hakuna huduma zozote anazozitoa kwa mdogo wangu… sasa angalieni
kweli huyu bwana alikuwa anampenda au amekuja leo kumharibia tu mwenzie
jamani,” alisema Rebeca.
Aidha, Paroko Msaidizi, Padri Richard D’saozi, alisema kwa kuwa wamekuja watu kutoa pingamizi na mambo hayo yapo kisheria zaidi hivyo anaiachia sheria ifuate mkondo wake
No comments:
Post a Comment