LULU AMPA SOMO MTOTO WA MIL. 50 ZA TMT
Stori: Shakoor Jongo MUIGIZAJI
mwenye mvuto wa aina yake katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth
Michael Kimemeta ‘Lulu’ amempa somo mshindi wa Shindano la Tanzania Move
Talent ‘TMT,’ Mwanafaa Mwinzago kuwa asibwetekena ushindi aliopata
bali azingatie masomo.
Akizungumza
na Ijumaa juzikati, Lulu alisema ni kweli binti huyo ana kipaji na
ilikuwa haki kushinda milioni 50 ila ajue bado ni mtoto na anatakiwa
kukomalia elimu.
“Ustaa
ni cheo kikubwa sana hasa katika jamii na kila mtu anakuangalia wewe,
ili ujikontroo unatakiwa ujitambue na huwezi kujitambua kama huna elimu
ya kutosha hivyo mimi namshauri aweke suala la masomo mbele kuliko
ustaa alioupata,” alisema Lulu.
Fainali za TMT zilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Ukumbi wa Mlimani City ambapo Mwanafaa aliibuka kidedea.
No comments:
Post a Comment