Uongozi wa klabu ya Young Africans leo
umewekeana sahihi ya makubaliano na Benki ya CRDB nchini juu ya
uboreshaji na utengenezaji wa kadi za uanachama, hafla hiyo imefanyika
katika Makao Makuu ya Benki hiyo eneo la Posta mpya jijni Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dr Charles Kimei
amesema anaushukuru uongozi wa Yanga kwa kuwaamini benki yao kuwa
wanaweza kufanya kazi hiyo, na sisi tunaamini tutafanya kazi vizuri na
kuweza kufikia malengo yao waliyotuwekea katika kipindi muafaka.
Kwetu sie kupata nafasi ya kufanya kazi na
klabu ya Yanga ni jambo jema, tunatambua wana wana wapenzi zaidi ya
milioni 20 nchi nzima, hivyo ni jukumu letu kuhakikisha tunawifikia kila
sehemu walipo na wanajiunga na uanachama wa kalbu yao pendwa alisema
“Dr Kimei”.
Aidha Kimei amesema kwa utaratibu huo wa
mfumo wa kisasa, wataanza kwa kutoa bure kadi za uanchama wa Yanga
ambazo zitakua na nembo ya VISA itakayomfanya mtumiaji aweze kuitumia
sehem yoyote alipo na kurahisisha zoezi la ukusanyaji wa ada za
uanachama.
Gharama ya kadi itakua ni Tshs 8,000 tu kwa
watakaoanza upya (bure kwa waliokua tayari wanachama) na
mteja/mwanachama ataendelea kuichangia klabu yake ya Yanga kiasi cha Tsh
250/= tu kwa wiki ambapo kwa mwezi ni sawa Tsh 1,000/= na kufanya kwa
mwaka ada kuwa ile ile Tshs 12,000/=.
Kwa upande wa mjumbe wa Baraza la Wadhamini
wa klabu ya Young Africans Bi Fatma Karume amesema anaishukuru benki ya
CRDB kwa kubali kufanya kazi hiyo, na kwa uwezo wao wa utendaji kazi
anaamini wataifanya kazi hiyo kwa kiwango cha hali ya juu.
“Kikubwa nilichofurahi ni kuwa hawa CRDB Bank
wapo mpaka kwetu Unguja, hivyo naona zoezi hilo litafanikiwa vizuri na
kurahisisha upatikanaji wa kadi za wanachama kwa uharaka zaidi alisema ”
Bi Fatma.
Kadi mpya za uanachama wa Yanga
zitakazotolewa na CRBD Bank zitakua za aina mbili, Premieum Visa Card
kwa ajili ya viongozii mashuhuri wa klabu ya Young Africans tangu
kuanzishwa kwake na nyingine ni Normal Visa Card kwa ajili ya wanachama
wa kawaida.
Awali klabu ya Young Africans ilikuwa na
mkataba wa aina hiyo na Benki ya Posta, Uongozi wa Yanga umeshawasilisha
Notice kwa benki ya Posta juu ya kusitisha mkataba nao na sasa huduma
hiyo itaanza kutolea kupitia benk ya CRDB.
Source: http://www.youngafricans.co.tz
No comments:
Post a Comment