Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa MH!
Hatimaye yule mwanaume aliyedaiwa kufumaniwa na mke wa mtu na hatimaye
kufanyiwa usodoma na watu sita, akiwemo mume wa mwanamke huyo
amefungukia mchezo mzima.
Hivi karibuni mwanaume huyo (jina tunalo) ambaye ni mume wa wake wawili na mkazi wa Yombo Kiwalani, Wilaya ya Ilala jijini Dar mwenye umri wa miaka 34 alikutwa na mkasa huo kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Yombo Executive inayomilikiwa na Athuman Maembe (pichani).
Hivi karibuni mwanaume huyo (jina tunalo) ambaye ni mume wa wake wawili na mkazi wa Yombo Kiwalani, Wilaya ya Ilala jijini Dar mwenye umri wa miaka 34 alikutwa na mkasa huo kwenye nyumba ya kulala wageni iitwayo Yombo Executive inayomilikiwa na Athuman Maembe (pichani).
Mara
baada ya picha za tukio hilo kuenea kwenye mitandao ya kijamii na watu
kushangaa, gazeti hili lilituma timu yake ya habari za uchunguzi ili
kupata ukweli wa tukio hilo.Uwazi lilifanikiwa kumpata mwanamume huyo
ambaye ni mfanyabiashara, pia alijitambulisha kuwa yeye ni mwelimishaji
rika wa magonjwa ya ngono, afya ya uzazi, madawa ya kulevya na
unyanyasaji wa kijinsia.
Alianza kwa kusema: “Ni
kweli mimi ndiye niliyetendewa ukatili ule. Natamani kujiua kwani mambo
yale nayasikia tu usiombe yakukute.
“Nimefedheheka sana, sina
mahala pa kuficha aibu hii kubwa. Kila nikikumbuka kuwa nina wake
wawili na watoto, wazazi, marafiki na ndugu, bora hata wangeniua kuliko kuniacha nazidi kudhalilika hivi.
“Siku ya tukio ilikuwa Jumamosi ya Agosti 23, mwaka huu. Kuna mwanamke mmoja anaitwa mama Lilly alinipigia simu. Kwanza alikuwa akinipigia simu mara kwa mara wiki moja kabla ya tukio akinieleza kwamba ana shida na mimi, alisema mume wake amekuwa akimnyanyasa kijinsia.
“Siku ya tukio ilikuwa Jumamosi ya Agosti 23, mwaka huu. Kuna mwanamke mmoja anaitwa mama Lilly alinipigia simu. Kwanza alikuwa akinipigia simu mara kwa mara wiki moja kabla ya tukio akinieleza kwamba ana shida na mimi, alisema mume wake amekuwa akimnyanyasa kijinsia.
“Siku hiyo, saa tatu asubuhi mama Lilly
alinipigia simu huku analia, akasema kwamba mumewe kampiga na
kumfukuza nyumbani hivyo anaomba kuonana na mimi kwa ajili ya ushauri
ila alitaka tukutane naye maeneo ya Mtongani, Mbagala au Tandika.
“Nilikataa, nikamwambia
aje kwenye Ukumbi wa Maembe ninakotoaga mafunzo mbalimbali kwa vijana.
Ukumbi huo upo karibu na nyumba hiyo ya kulala wageni kulikotokea
tukio.
“Huyu mwanamke namfahamu kwani kipindi cha nyuma alikuwa na stationary karibu na maeneo haya, nilikuwa nikimtengenezea kompyuta lakini miaka miwili iliyopita alihama na sikujua alipo hadi hivi karibuni aliponipigia simu.
“Huyu mwanamke namfahamu kwani kipindi cha nyuma alikuwa na stationary karibu na maeneo haya, nilikuwa nikimtengenezea kompyuta lakini miaka miwili iliyopita alihama na sikujua alipo hadi hivi karibuni aliponipigia simu.
“Basi, nilipomwambia aje
yeye maeneo haya, aliamua kunifuata. Alifika saa saba mchana huku
akibubujikwa machozi, nilimsikiliza kwa makini matatizo yake mwishowe
aliniomba nimkopeshe shilingi laki moja ili aende kwao, nilimjibu kwa
pale sikuwa nazo labda mpaka Jumatatu.
“Akasema kama ni hivyo
basi nimsaidie sehemu ya kulala ili kesho yake aondoke kwenda kwa dada
yake. Nilimuonea huruma, nilimchukulia chumba, nikamwambia kama
kutakuwa na tatizo anipigie simu. Wakati najiandaa kutoka chumbani
aliendelea kuongea maneno mengi sana ya kunifanya niendelee kuwepo.
“Wakati huo alikuwa
akituma ujumbe wa simu sehemu nisiyoijua. Sasa nilipoagana naye, ile
natoka tu, mlangoni niliona wanaume sita wakanirudisha chumbani na
kufunga mlango.“Wakaniambia niwape namba yangu ya akaunti ya benki na
password ya simu yangu kwani walijua kwamba tayari nimetumiwa fedha
kutoka nje ya nchi kutoka kwa wafadhili.
“Niliwaambia sina
akaunti, wakanipiga sana, ikabidi niwaongopee kwamba nyumbani nina
shilingi laki tano, wakaniambia niwaelekeze nyumbani, nikafanya hivyo.
Wawili kati yao waliondoka na pikipiki hadi kwangu kuchukua fedha,
wengine wakawa wamenizuia chumbani na kunitishia nikipiga kelele ndiyo
mwisho wa maisha yangu.
“Wale walipofika kwangu
walimwambia mke wangu awape laki tano na walimtaka aongee na mimi kwa
simu huku nikiwa chini ya ulinzi. Mke wangu aliwaambia hana fedha hizo
ana laki moja tu, nilimwambia awape.“Waliporudi na shilingi laki moja
walisema nimewadanganya, wakaniadhibu na kunivua nguo, wakanilawiti
kwa zamu na kunilazimisha kuwafanyia mambo ambayo ni tabu hata kuyasema
huku wakinipiga picha.
“Baada ya kumaliza walichukuwa laptop,
nguo na simu wakaondoka huku wakiniambia ifikika Jumatatu, yaani siku
moja baada ya tukio niwape shilingi milioni moja la sivyo wanaweka
picha zangu mtandaoni.
“Hata hivyo, baada ya
kukosa hizo fedha waliziweka picha mtandaoni, ikawa napigiwa simu na
watu mbalimbali walioziona.“Waliponiacha pale chumbani nikiwa sina
nguvu, nilichukuwa shuka nilijikokota mpaka kwa meneja wa gesti na
kumweleza. Alinipa nguo yake ili niweze kwenda Kituo Kidogo cha Polisi
cha Minazi Mirefu kutoa taarifa na baadaye Buguruni na kufungua kesi
yenye jalada namba BUG/RB/8520/2014 Kujipatia Fedha kwa Njia ya
Udanganyifu lakini baadaye ikaongezwa shitaka lingine la kulawiti.
“Kinachonishangaza ni kwamba iweje wanaume hao sita waingie na kutoka bila wenye gesti kuwabaini?” alihoji mwanaume huyo.
Naye mmiliki wa nyumba
hiyo ya wageni alikiri kupokea taarifa ya kutokea kwa tukio hilo na
kudai kwamba ni la aibu na kusema suala hilo linashughulikiwa na jeshi
la polisi.
Kamanda wa Mkoa wa
Kipolisi Ilala, SACP, Mary Nzuki alipohojiwa na mmoja wa waandishi wa
habari hii ofisini kwake mwishoni mwa wiki iliyopita alikiri kutokea
kwa tukio hilo na kusema tayari watuhumiwa wanne wanashikiliwa Kamanda Nzuki aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Erick Kasila, Sanifa Sadik, Shela Sadik na Juma Richard.
No comments:
Post a Comment