Tuesday 2 September 2014

MWANAMKE AGONGWA NA DALADALA UBUNGO MAJI


Raia wakijaribu kuokoa maisha ya dada aliyegongwa na gari (daladala) maeneo ya Ubungo maji wakati akivuka bara bara.
Majeruhi akichukuliwa kwenye gari na wasamaria wema.
HiIi ndilo gari aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T454 BBV lililomgonga dada huyo.

Mwanamke mmoja (jina halijafahamika) aliyekuwa anavuka barabara ya Morogoro maeneo ya Ubungo maji kutoka ng'ambo ya tank na kuelekea upande wa Tanesco amegongwa na gari ya daladala aina ya Toyota Coaster lililodaiwa kuvunja sheria likiwa  linapita kwenye barabara ya magari ya mwendo kasi.
Katika ajali hiyo dereva wa basi(daladala) hakupatikana kwani alikimbia baada ya ajali

No comments:

Post a Comment