Waziri mkuu wa Lesoto Thomas Thabane amewasili nchini mwake baada ya jaribio la kutaka kumpindua.
Bwana Thabane alikimbilia Afrika Kusini siku ya Jumamosi saa chache baada ya wanajeshi kukaribia ikulu yake na kudhibiti vituo vya polisi.
Ripoti zinasema kuwa polisi wa Afrika Kusini kwa sasa ndio wanalinda nyumba za waziri mkuu huyo na naibu wake
Thabane (70) aliwasili Lesotho saa 6 mchana
nchini Lesotho na leo viongozi wa vyama vyote 3 vinavyo unda serikali ya
mseto ya Lesotho vinatarajiwa kukutana na mfalme wa nchi hiyo Letsie
kumuarifu yaliojiri J3 A-Kusini kwenye mkutano wao waku upatanishi
ulioongozwa na rais Jacob Zuma.
Suala la kulifungua tena bunge la Lesotho
lilofungwa na waziri mkuu tangu mwezi Juni ni miongoni mwa mada zitakazo
wasilishwa mbele ya
mfalme Letsie na shirika la maendeleo la nchi za kusini mwa Afrika SADC
ambalo lilimtaka waziri mkuu na naibu wake Metsing walifungue bunge
hilo mwezi huu.
Kwa sasa hali ya utulivu inaonekana kuwepo
katika mjii mkuu wa Maseru huku Askari polisi wa A-Kusini wakilinda
makazi ya waziri mkuu na naibu wake .
Badhi ya repoti zinasema endapo bunge la Lesotho
litafunguliwa tena huenda waziri mkuu Dr Thomas Tabane akapigiwa kura
ya kutokua na imani nae .
No comments:
Post a Comment