Mlipuko wa moto Jomo Kenyatta wa mwathiri Diamond Platnum
MSANII wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond Platnum’ ni mmoja wa abiria walioathiriwa na moto uliowaka jana asubuhi katika eneo la maegesho ya abiria kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), jijini Nairobi.
Kwa mujibu wa Meneja wa msanii huyo nyota nchini, Bob Tali, mteja wake alikuwa akirejea nchini akitokea Afrika Kusini ambako alikwenda kwa ziara ya kimuziki.
Tali alisema msanii huyo alikuwa aunganishe ndege kutoka Nairobi hadi Dar es Salaam, lakini alishindwa asubuhi kutokana na moto huo uliowaka uwanjani hapo kuanzia asubuhi.
Alisema wakati moto ukitokea, Diamond alikuwa uwanjani hapo akisubiria kuanza kwa safari yake.
Alisema kutokana na moto huo ambao umedhibitiwa, Diamond Platnum alilazimika kukaa jijini Nairobi kwa muda mrefu na alipangiwa kuondoka baadaye jana jioni, baada ya kuanza tena kwa safari baada ya kusitishwa na baadhi ya safari kuanzia kwenye Uwanja wa Ndege wa Mombasa, Pwani ya Kenya.
No comments:
Post a Comment