NI siku nyingine tunakutana katika ukurasa wetu wa kupeana mambo muhimu ya kuboresha uhusiano wetu na wapenzi wetu. Nawashukuru wasomaji wetu wote ambao wamekuwa wakinipa moyo kwa kunitumia ujumbe mfupi wa maneno na wengine kunipigia moja kwa moja !
Baada ya utangulizi huo, sasa tugeukie katika mada yetu la leo.
Hebu jiulize; mpenzi wako anapokuambia anakupenda, inatosha kweli kukuthibitishia kuwa anakupenda kwa dhati na uendelee kumwamini? Hapa kila mmoja anaweza kuwa na jibu lake lakini kwa wataalamu wa Saikolojia ya Mapenzi hawakubaliani na hoja hii.
Kwa nini? Kwa sababu neno nakupenda ni jepesi sana katika hali ya kawaida kutamkika lakini lina maana kubwa sana linapokuja katika ulimwengu wa mapenzi ya dhati.
Naam! Ulimwengu wa mapenzi ya dhati kwa sababu kuna wengine hawana mapenzi ya kweli wanapotamka neno hili. Wanasaikolojia wa masuala ya uhusiano wanaeleza kwamba neno hilo linaweza kuwa na maana ikiwa litalandana na matendo.
Wengi wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu katika uhusiano. Wapenzi wao wamekuwa hawaeleweki kama wana mapenzi ya kweli au la, kutokana na mambo wanayowafanyia lakini wakati huo huo neno nakupenda limekuwa halikauki midomoni mwao.
Ni haki yao kuchanganyikiwa lakini kuchanganyikiwa huko kunatokana na kutokujua mambo ya uhusiano vyema. Mpenzi msomaji wangu, inawezekana wewe ukawa mmoja wa watu hao, hii ni nafasi yako mahususi kwa ajili ya kumfahamu mpenzi wako vyema.
Kwa nini uhifadhi moyo wako kwa mpenzi asiye na mapenzi ya kweli? Je, utajuaje kama mwenzi uliyenaye ana penzi la dhati moyoni mwake? Hebu tuone vipengele vifuatavyo;
ANAKUPUUZA...
Hili ni tatizo kubwa katika uhusiano na hasa kwa wasichana. Wanaume wengi wa siku hizi ambao wana mapenzi ya ubabaishaji huwapuuza wenzi wao.
Hivi utawezaje kukubali kuendelea kuitwa mpenzi na kila wakati mtu huyo anakuambia anakupenda lakini anakupuuza? Bado utaendelea kumhesabia mtu huyo anakupenda? Kwa lipi hasa wakati hazingatii yale unayomwambia hata kama yana msingi kiasi gani katika maisha yenu yajayo ?
Mpenzi mwenye mapenzi ya kweli, kwanza huzingatia mawazo ya mpenzi wake, hupima kila aambiwalo na kulifanyia kazi. Huwezi kumpuuza mtu ambaye unampenda hata siku moja. Hiki ni kipimo cha kuzingatia wakati wa kutafuta mpenzi wa kweli.
Hata kama anakuambia anakupenda mara ngapi kwa siku, lakini kama haoneshi kuthamini umuambiayo, penzi la mtu wa aina hii lina mushkeli.
Anayekupenda huwa makini kukusikiliza kwa kila kitu. Mwingine anaweza akawa anamshauri vizuri sana juu ya maisha lakini mwanaume huyo akawa hana ‘time’ kabisa naye.
Usingoje kujidhalilisha zaidi ya hapo, huyu atakuwa hakupendi ila ana vitu anavyovipata kwako ndiyo maana anajilazimisha kukuambia ‘nakupenda’ ya kinafiki ili aendelee kupata anachokipata kutoka kwako. Upo hapo ?.
ANAHOFIA SIMU YAKE.
Hapa kuna utata mkubwa! Wengi hujitetea kuwa simu ya mkononi ni kwa ajili ya mhusika na siyo vinginevyo. Hapa kuna ukweli fulani lakini wengi walio katika uhusiano hutumia kijisababu hiki kama nguzo ya kuendelea kufanya mambo yao yasiyofaa kwa kutumia simu zao.
Hata hivyo, wanasaikolojia ya mapenzi wanaunga mkono hoja hiyo, maana wakati mwingine unaweza ukachukua simu ya mpenzi wako, ikasababisha mgogoro mkubwa.
Pamoja na hilo, kumgundua mwizi ni rahisi sana, ukikutana naye hata kama humfahamu unaweza ukajikuta unamhisi, ndivyo ilivyo katika uaminifu wa simu za mikononi. Ukiona umeshika tu simu yake anakuwa mkali, jua kuna kitu kinaendelea.
Simu inapigwa halafu ghafla anatoka kwenda kupokelea nje, jiulize mara mbili. Lakini wakati mwingine ukiona simu yake inaita halafu jina linalotokeza kwenye simu yake lina utata, anza kufikiria mara mbili.
Kwa mfano uliona jina limeandikwa: G45, BM, Chizi, Magomeni, Jumapili na majina mengine yenye utata au yaliyofupishwa, jua kuna mambo yanaendelea chini ya kapeti !.
Ukianza kuhisi tofauti kidogo juu ya simu yake, anza kumchunguza na mara nyingi akigundua unamchunguza kuliko umharibie mambo yake atakuwa tayari kuachana na wewe. Kukuambia anakupenda pekee hakutoshi kwa kasoro hii.
HATAKI KUKUTAMBULISHA!
Kukupenda kwake hakuwezi kukamilika ikiwa hataki kukutambulisha.
Ni kweli kwamba jambo hili siyo la haraka lakini unaweza kukuta wapenzi wapo katika uhusiano kwa mwaka mzima au zaidi lakini hakuna ndugu yeyote wa upande wa mwanaume anayemfahamu! Ukiachilia mbali ndugu lakini hata rafiki zake wa karibu hawamfahamu, hilo ni tatizo.
Kwa hali kama hiyo hata kama jamaa atakuwa akirudia kusema anakupenda mara ngapi, ana mapenzi ya kweli? Hakika hakuna.
Dada zangu wapendwa, wanaume wamejaliwa sana ujuzi wa kuongea, ndimi zao ni tamu zisizokaukiwa na maneno lakini hayo huyazungumza wakiwa na malengo na mipango yao ambayo inaweza kufanikiwa akiwa na wewe.
Kwa misingi hiyo atashindwaje kukuambia anakupenda hata kama ni mara mia tisa tisini? Siyo kazi kusema nakupenda kutoka mdomoni lakini inapokuja maana ya neno hilo kutoka moyoni ndiyo shughuli inapoanzia.
Kwa leo naweka kituo kikubwa hapa, wiki ijayo usikose katika sehemu ya
No comments:
Post a Comment