Wednesday, 27 August 2014

Flora Mbasha,Nina Mimba ya Mbasha sio Gwajima

Flora Mbasha,Nina Mimba ya Mbasha sio Gwajima


Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania ambae pia ni Mke wa Emmanuel Mbasha amefunguka na kusema kuwa hana mahusiano yoyote ya kimapenzi na na Mchungaji wa Kanisa la kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima,
Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Flora Mbasha
Flora amesema hayo leo alipokuwa akichat Live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kuanzia saa Sita kamili.
Flora amesema kuwa hawezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu ambae ni ndugu yake hivyo Mchungaji Gwajima ni mjomba wake na si mpenzi wake kama ambavyo watu wamekuwa wakizusha kwa lengo la kumchafua na kumshushia hadhi."Hayo ni maneno tu ya watu mtaani ila Mchungaji
Gwajima ni mtumishi wa Mungu na ni uncle wangu ninawezaje kuwa na mahusiano na uncle wangu..? "Alihoji Flora.
wakati akijibu ya maswali ya mashabiki ambayo mengi yao yalikuwa yakimtuhumu na huku watu wengi wakitaka kujua ukweli juu ya ugomvi uliopo kati yake na Mumeo kama ni kweli au ni skendo tu za magazeti,Flora aliweka wazi kuwa kuna vyombo vya habari ambavyo vimekuwa na lengo la kumchafua na kumualibia sifa ndio maana walitumia gharama kubwa kufanya wanavyoweza ili kutimiza malengo yao,mbasha amedai kuwa alimua kukaa kimya kwa kuwa hakukuwa na ukweli wowote.
"Hizo stori mnazosikia hazina ukweli wowote na ndio maana niliamua kukaa kimya sikutaka kujibizana kwenye vyombo vya habari kwa uongo wa
baadhi ya magazeti ya udaku ila ninasikitika sana kwani kuna watu wamekaa na kujipanga kisawa sawa kwa ajili ya kuhakikisha wanaharibu huduma yangu kwa gharama zozote, lakini bado ninasonga mbele kwani mwanzilishi wa huduma yangu ni Mungu na huyo ndiye atakayeimaliza na sio mwanadamu. hata hivyo ninawashukuru kwa kuwa wamenitabilia nkuja kumiliki jumba na magari ya kifahari ingawa yote ni ubatili"
SIJAACHANA NA MBASHA KISA GWAJIMA
Flora Mbasha amesema kuwa watu wengi wanasema kuwa ameachana na Mumewe kisa Gwajima hilo swala halina ukweli wowote hajaachana na Mbasha sababu ya Gwajima na amedai kuwa bado anampenda sana ila anampenda Mungu zaidi.bali amekuwa na matatizo katika ndoa yake kati yake na mumewe na ni matatizo yao ya ndani ambayo asingependa kuyaweka wazi katika vyombo vya habari maana kufanya hivyo ni sawa na kumvunjia heshima mumewe,maana mambo ya chumbani ni siri yao wenyewe asingependa kuwa wazi sababu wanamtoto mkubwa sasa.
"Sijamwacha mume wangu sababu ya Gwajima na kweli bado napenda sana Mbasha lakini nampenda zaidi Mungu"
Wakati anazungumzia suala hili Flora ameweka wazi kuwa kwa sasa ni mjamzito na ujauzito huo ni wa Mume wake ambae ni Emmanuel Mbasha maana ameishi nae katika ndoa zaidi ya miaka kumi na katika kipindi chote hicho hajawahi hata siku moja kumsaliti Mumewe na kwenda kwenye michepuko hivyo huo ujauzito ni wa Mume wake Emmanuel Mbasha na siyo Gwajima.

No comments:

Post a Comment