Friday 8 August 2014

Mawakili wa Oscar Pistorius viongozi wa mashitaka wamevuruga kesi


Kundi la mawakili wanaomtetea mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius wanasema kuwa viongozi wa mashitaka wamevuruga kesi hiyo kwa minajili ya kumfanya kuwa na makosa

Kwenye taarifa yake ya mwisho wakili wa Pistorius Barry Roux amesema kuwa bwana Pistorius angefunguliwa mashitaka ya kuua bila kukusudia bali si ya mauaji baada ya kumpiga risasi na kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.

Lakini bwana Roux alikiri kwamba Pistorius anapaswa kupatwa na hatia kwa kosa la kutumia silaha yake katika mgahawa.Bwana Pistorius anasema kuwa alimpiga risi kimakosa akidhani kuwa alikuwa ni jambazi.
Wakati kila upande utakapokamilisha kutoa kauli zao ya mwisho jaji ataahirisha kesi hiyo kwa takriban wiki moja kufanya uamuzi.
Mwanariadha huyo amekanusha makosa yake dhidi yake ikiwemo kosa la kutumia silaha yake katika sehemu ya umma pamoja na kumiliki silaha haramu.

No comments:

Post a Comment