Kwenye Kituo cha Polisi cha Maturubai kilichopo Mbagala, Dar kuna faili
la kesi namba MBL/RB/ 9817/2014- KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI ambalo
linamsaka kijana Juma Athumani (30), mkazi wa Charambe, Mbagala kwa kosa
la ubakaji wa denti wa darasa la saba. Habari za kiintelijensia zilidai kwamba mtuhumiwa huyo ambaye ni muuza genge, alitenda kosa hilo Agosti, mwaka huu ambapo denti huyo alikuwa ametumwa na mama yake gengeni.Ilisemekana kwamba jamaa huyo alimuomba denti huyo wazungumze kidogo ndipo akampeleka gesti kwa lazima.
Akizungumza na gazeti hili bora la habari
za mastaa na kijamii, denti huyo alisema kuwa alipofika gesti, jamaa
huyo alilipa fasta na kumvutia chumbani ambapo alianza kumshika ‘manido’
kisha akamtupia kitandani na kumwingilia kimwili bila ridhaa yake.
Mama wa mwanafunzi aliyebakwa.
Alisema kwamba, jamaa alipomaliza
shida zake, alimpa buku tano (5,000/=) lakini alipokataa huku akilia
ndipo mwanaume huyo akamuongezea hadi ikafika buku kumi (10,000/=).
“Niliporudi nyumbani mama
aliniuliza kwa nini nimechelewa kisha akaziona hela, akaniuliza
nimezipata wapi, nikamwambia amenipa Juma ndiyo tukaenda hadi gengeni
kwa Juma kuuliza ndiyo mama akagundua kuwa nimebakwa.
“Baadaye mama alikwenda kuripoti
polisi ndipo Juma akakamatwa na mimi nikapelekwa hospitali na
kugundulika kweli nilikuwa nimebakwa,” alisema denti huyo.
Habari zilizotufikia punde kabla ya
kuingia mitamboni zilidai kwamba uchunguzi wa polisi unaendelea ili
sheria ichukue mkondo wake.
No comments:
Post a Comment