Wednesday, 27 August 2014

ODAMA ASHEREHEKEA BETHIDEI YAKE NA WATOTO YATIMA MAUNGA, DAR

MSANII wa Bongo Muvi, Jenipher Kyaka ‘’Odama’’,  jana alifanya sherehe yake ya kuzaliwa kwa kutoa msaada katika kituo cha watoto yatima cha Maunga, kilichopo  Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Sherehe hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Vijana Mwananyamala, Dar es Salaam, ilihudhuriwa na wasanii kibao wakiwamo Johari, Mayasa, Cathy, Shamsa Ford, Chuchu Hans, Monalisa, Yusuph Mlela, Steve Nyerere, Chichi  na wengineo.
Odama ambaye pia alikuwa na familia yake alitoa zawadi mbalimbali kwa watoto hao ikiwa ni pamoja na chakula, sabuni na vinginevyo pamoja mbali  na kula na kunywa na watoto hao.

No comments:

Post a Comment